|
Afisa Elimu wa Halmashauri ya Longido
Ndg. Gerson Mtera(mbele) akisoma taarifa ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya Longido wakati wa ziara ya Mkuu
wa Mkoa wilayani hapo.
|
|
Ujenzi unaendelea katika mabweni ya
Shule ya Sekondari Longido na hivi ndivyo yanavyoonekana kwa sasa.
|
![]() |
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Gambo(kwanza kulia) akishirki kwenye ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari
Longido.
|
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Gambo(aliyesimama) akizungumza na walimu pamoja na watumishi wasio walimu
katika Shule ya Sekondari Longido wakati wa ziara ya Kikazi Wilayani hapo.
|
|
Mkuu w Wilaya ya Longido Mhe. Daniel
Chongolo akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa
kikao na walimu wa Shule ya Sec. Longido.
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo
amechangia mabati 136, mifuko ya Saruji 30 pamoja na Fedha taslimu Tsh 500,000
kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa mabweni mawili yaliyoungua moto hivi
karibuni katika Shule ya Sekondari Longido.
Rc Gambo ametoa msaada huo wakati wa ziara yake ya Kikazi wilayani hapo ambapo alitembelea Shule
hiyo na kukuta wanafunzi wakilala madarasani tangu Mabweni hayo yalipoungua na
uongozi wa Shule hiyo kuamua kutumia madarasa hayo katika kipindi hiki cha
mpito wakati wakiwa wanaendela na ujenzi
wa mabweni hayo ambayo ujenzi wake unagharimu zaidi ya Tsh Mil 45.
Akisaoma taarifa ya ujenzi wa mabweni hayo Afisa Elimu
Sekondari Bw.Gerson Mtera alisema endapo wangetumia Mkandarasi ujenzi huo
ungegharimu zaidi ya Ths Mil 75 lakin kwa kuwa wanajenga kwa kutumia mafunzi wa
jamii pamoja na wataalamu wa Halmashauri mabweni hayo yatagharimu Tsh Mil 45
tu.
Nimeona jitihada za uongozi wa Wilaya pamoja Shule
katika kukabiliana na changamoto hii na jitihada zenu hakika sio za kupuuzia na
mimi kama Kiongozi wa Mkoa nawiwa kuchangia kazi hii ili iweze kukamilika
haraka na wanafunzi warudi katika malazi yaliyo bora na madarasa hayo yaweze
kutumika kwa shughuli stahiki alisema
Gambo.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa alikutana na walimu pamoja
na wafanyakazi wasio Walimu kusikiliza
malalamiko na kubaini baadhi wa walimu kutolipwa malimbikizo ya Fedha za Likizo
pamoja na watumishi kuajiwa kwa zaidi ya miaka kumi pasipo kuwa na mkataba wala
barua ya ajira kutoka kwa Mwajiri wake.
Akiongea katika Kikao hicho Mhe. Gambo alisemani ni
muhimu kwa kila Halmashauri kuwajali watumishi wake haswa walimu na wafanyakazi
wa kada za chini ili kuwaongezea ari ya kufanya kazi na kuwatia moyo waweze
kutumikia Taifa hili kwa uzalendo sio kila siku mnatoa vipaumbele kwa watumishi
wa Kada za juu kufanya hivi mnasababisha matabaka yasiyo ya lazima katika
utendaji kazi wenu wa kila siku.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo aliahidi
mbele ya Mkuu wa Mkoa kuwa atasimamia ipasavyo wote wanaohusika na ujenzi wa
mabweni ya Sekondari ya Longido ili kukamilika kwa wakati na kwa ubora
unaotakiwa na kumhakikishia kwamba mpaka mitihani ya Kidato cha nne itkapoanza
wanafunzi hao watakua wameshahamia kwenye Mabweni hayo na madarasa hayo
yatatumika kwa ajili ya kazi hiyo na baadae wanafunzi wataendelea kuyatumia
katika masomo yao.
Pia aliongeza kuwa atafuatilia malimbikizo ya Fedha za
waalimu wanazodai kwa ajili ya Likizo ili kuangalia uwezekano wa kuwalipa
kutoka katika Mapato ya Halmashauri na kuwaagiza Mkurugenzi wa Halmashauri
kushushulikia malalamiko ya watumishi wote ambao hawana barua za ajira hadi
sasa.
Kuanzai wiki ijayo Mkurugenzi pamoja na Menejiment ya
Wilaya kupitia vikao vyenu mliangalia suala hili kwa makini na Bodi ya Ajira
iweze kuketi ili watumishi hawa waweze kupata haki yao.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo yuko katika
muendelezo wa ziara yake ya Kikazi katika Wilaya ya za Mkoa wa Arusha amabapo
mpaka sasa amekwisha tembelea Wilaya ya Ngorongoro.
WANAFUNZI WA LONGIDO SEKONDARI MWISHO KULALA MADARASANI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 25, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment