MADIWANI wanne akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha wafikishwa mahakama ya mwanzo Enaboishu Wilayani Arumeru.


Mahakama ya mwanzo ya Enaboishu iliyopo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha Jana imewasomea mashtaka madiwani wanne akiwamo mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha Noah Lembris.

Aidha katika mashtaka yaliyosomwa mbele ya Hakimu David Dhahabu yalieliza kuwa viongozi hao wakabiliwa na shtaka la kutoa lugha ya kashfa kwa mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti.

Askari aliyesoma mashtaka hayo alisema madiwani hao walitoa lugha za kashfa kuwa "mkuu wa Wilaya siyo polisi,nyingine Serikali ina  ubabe katika kutekeleza majukumu ya CCM.

Kashfa nyingine "mkuu wa Wilaya anatumia  masaa masaa 48 kuwaweka viongozi ndani ambapo wahishtakiwa walikana  mashtaka hayo kuwa si ya kweli.

Hata hivyo mashtaka hayo yanaeleza kuwa kutoa lugha za kashfa kwa viongozi ni kinyume cha sheria kwa mujibu  wa kifungu cha sheria cha 89 kifungu kidogo cha 16 kanuni ya adhabu ambapo ilifanyiwa marekebisho 2002.

Baada ya hakimu Dhahabu kusikiliza mashtaka hayo alimtaka askari huyo aliyesoma mashtaka hayo kumwandikia barua ya kumtaka  mlalamikaji kufika mahakamani siku ya kusikilizwa  kwa kesi hiyo.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa  mapema oktoba 24 majira ya saa  3:00 ambapo washtakiwa  wapo nje kwa dhamana ya  laki 5 kwa kila mmoja na wadhamini wawili.

Waliofikishwa mahakamani hapo ni pamoja na Mwenyekiti wa 
Halmashauri ya Arusha Noah Lembris, Happy Gadiel Diwani Viti maalum, Winfrida Lukumay na Nuru Ndosi.
Wakiongea  nje ya mahakama hiyo viongozi hao walisema  ni uonevu na ukandamizaji wa haki za binadamu walichofanyiwa.
Mwenyekiti Lembrisi alisema mkuu wa Wilaya ameamua kuwadhalilisha Chadema ambapo alisema nikudhohofisha chama.
"Pamoja na kutaka kutudhohofisha 
Chama sisi hatutarudi nyuma maana tunaamini  hawezi kufanikiwa kutudhohofisha kwa sheria zake kandamizi anazozileta"
alisema Lembrisi.
Alisema wanasikitika kusikia  mkuu huyo anajiita rais wa Arumeru wakati nchi hii inaongozwa na rais mmoja tu ambaye ni John Magufuli.

" Nia ya  Dc ni kuvuruga  juhudi za maendeleo  zinazofanywa na viongozi wa Chadema ila tunamwambia sisi anapotuweka mbali ndivyo anavyozidi kutufanya tuwe ngangari kwa kupambana zaidi kuwaletea wananchi maendeleo " alisema .

Aliongeza kuwa hadi sasa wenyeviti zaidi ya saba wa maeneo mbalimbali ya Arumeru wapo ndani kwa masaa 48 kutokana na amri ya mkuu huyo wa Wilaya.
Naye mwanasheria wa Chadema Charles Abraham alisema anashangazwa na  vitendo vya Dc vya kuingilia kazi za madiwani kwani siyo sheria kuomba ruhusa kufanya shughuli za maendeleo kwa wananchi wao.
" Rai yangu kwa rais ni kwamba anapoteua viongozi wa kuongoza  Wilaya aangalie vigezo zaidi watu wasiojua sheria hawawezi kuongoza  watu" alisema.

Alisema hakuna sheria iliyooanishwa katika kesi iliyopelekwa mahakamani inayowatuhumu viongozi hao hivyo ni kesi ambayo haieleweki.

"Sisi kama chama tunalaani vikali vitendo anavyovifanya kiongozi huyu na sidhani kama anafaham sheria  kuna maslahi yoyote mapana ya taifa yaliyoingiliwa ili apate kuwatuhumu vizuri " alihoji.

" Hata kama anaisoma sheria huenda haielewi maana haiwezekani kama  viongozi wana tekeleza majukumu ya kimaendeleo  yeye atoe amri wakamatwe badala ya kuungana nao kuleta maendeleo" alisema mwanasheria huyo.

Alisema wao kama chama wanachukua hatua za kisheria kuomba kesi ihamishiwe mahakama ya Wilaya ili  ipate  kusimamiwa na mawakili.

Kwa upande wake Diwani Viti maalum ambaye ni mshtakiwa Happy Gadiel alisema ni nguvu nyingine wanayo ongezewa kwa kuwekwa ndani kutokana na kuwatumikia wananchi waliowachagua.

"Ninawaambia tu wananchi wangu kuwa sitakata tamaa kutafuta maendeleo kwa sababu ya aina yoyote ile sisi tumejipanga na maendeleo yatakuja tu" alisema Gadiel.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa kijiji cha Kimyaki  kilichopo Wilayani hapo alifikishwa Mahakaman kwa kosa hilo hilo la kutoa lugha zakashfa kwa mkuu huyo wa Wilaya.

Mwenyekiti huyo jina  Alphayo Michael alisomewa mashtaka ya kutoa kashfa kwa Dc   katika mkutano wake  na wana kijiji uliofanyika  agost 8 mwaka huu.
Jambo hilo limewashangaza waliohudhuria Mahakamani kutokana na mashtaka kufanana huku viongozi hao wakiwa wanatokea maeneo tofauti.
MADIWANI wanne akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha wafikishwa mahakama ya mwanzo Enaboishu Wilayani Arumeru. MADIWANI wanne akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha wafikishwa mahakama ya mwanzo Enaboishu Wilayani Arumeru. Reviewed by KUSAGANEWS on October 17, 2016 Rating: 5

No comments: