TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHESHIMIWA UMMY A. MWALIMU KUHUSU HUDUMA ZA MATIBABU KWA WATU WENYE ULEMAVU WASIO NA UWEZO
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy A. Mwalimu anapenda kutoa ufafanuzi kuhusu Tamko la Shirikisho la Watu
Wenye Ulemavu nchini (SHIVYAWATA) kuhusu makundi ya wananchi wanaostahili
kupata msamaha wa matibabu. Aidha,
baadhi ya Vyombo vya habari vimenukuu maelezo ambayo yametolewa na
mwenyekiti wa SHIVYAWATA kuhusu Makundi yanayostahili kupata msamaha wa
Matibabu nchini.
Kutokana na Maelezo hayo, napenda kutoa ufafanuzi ufuatao; Sera ya Afya ya Mwaka (2007) inatambua kuwa wapo wananchi ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kuzifikia huduma za Afya wakiwemo watu Wenye Ulemavu. Aidha, Kwa Sheria ya Watu Wenye Ulemavu Na.9/2010 ambayo, pamoja na mambo mengine, Sheria inabainisha kuwa Watu Wenye Ulemavu wana haki ya kuondolewa vikwazo katika kupata huduma za Afya.
Kwa kuzingatia maelekezo ya Sera ya Afya (2007) na Sheria ya Watu Wenye Ulemavu(2010) Wizara yangu inatambua na itaendelea kuhakikisha kwamba Watu Wenye Ulemavu Wasio na Uwezo wa kugharamia huduma za Matibabu wanapatiwa Msamaha wa Matibabu katika Ngazi zote kuanzia Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Mikoa na Hosptali za Rufaa.

Pia kwa kutambua umuhimu wa
huduma ya Afya kwa Wananchi wote, Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ipo katika mchakato wa kutungwa kwa sheria itakayowezesha
wananchi wote wakiwemo Watu Wenye Ulemavu kupata Kitambulisho cha Bima ya Afya.
Hatua hii itawaondolea vikwazo, wananchi wote wakiwemo watu Wenye Ulemavu katika
kuzifikia huduma za Afya pasipo kikwazo cha ukosefu wa fedha.
Naomba kuchukua fursa hii kuwahakikishia ndugu zangu Wenye Ulemavu kuwa wanayo haki ya kupata huduma za matibabu katika ngazi zote. Aidha, Serikali itaendelea kusimamia na kuhakikisha makundi maalum wakiwemo watu Wenye Ulemavu ambao hawana uwezo wa kuchangia huduma za Matibabu wanapata msamaha wa matibabu katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya.

Natoa maelekezo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwatambua Watu Wenye
Ulemavu Wasio na Uwezo wa kuchangia huduma za matibabu na kuimarisha Kitengo
cha Huduma za Ustawi wa Jamii katika vituo vya kutolea huduma za Afya ili
viweze kuwatambua na kutoa msamaha kwa watu wenye ulemavu wasio na uwezo
ili waweze kupatiwa matibabu bila ya vikwazo vya ukosefu wa fedha.
Aidha, ni marufuku kwa Mtumishi yeyote wa Sekta ya Afya kuonesha
vitendo vyovyote vya unyanyapaa na unyanyasaji kwa Watu Wenye Ulemavu wanaofika
katika vituo vya kutolea huduma za afya. Mtumishi atayethibitika kuonesha
kwenda kinyume cha maadili ya utumishi wa umma na taaluma za Afya kwa kufanya
vitendo vya vya unyanyapaa na unyanyasaji kwa makundi maaalum ikiwemo
watu wenye ulemavu atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa
kazi.
Wizara yangu inafanya jitihada kuhakikisha kuwa inaondoa vikwazo vyote vinavyowanyima watu wenye ulemavu kupata huduma za afya wanazohitaji ikiwemo kuhakikisha kuna mazingira mazuri yanayowawezesha kufika hospitali kwa kuweka miundo mbinu rafiki kwa watu wenye ulemavu. Vile vile, ninawataka watoa huduma wote kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu wanapofika hospitali.
Wapatiwe huduma haraka ili
kuwapunguzia usumbufu kutokana na mahitaji yao ya kimwili. Kama ambavyo
tumefanya kwa Wazee niwaagiza kila kiongozi ahakikishe anaweka utaratibu mzuri
wa kuwapa nafasi ya kwanza watu wenye ulemavu tukijifunza kwa jinsi
tulivyofanya na kufanikiwa katika eneo la kuhudumia wazee.
Watu wenye ulemavu ni wenzetu, watoto wetu, ndugu na jamaa zetu. Tuwahudumie kwa upendo na kuhakikisha wanapata fursa sawa na wengine
Watu wenye ulemavu ni wenzetu, watoto wetu, ndugu na jamaa zetu. Tuwahudumie kwa upendo na kuhakikisha wanapata fursa sawa na wengine
Imetolewa na
MHE. UMMY A. MWALIMU (Mb.)
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto
15/10/2016
TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII JINSIA, WAZEE NA WATOTO, MHESHIMIWA UMMY A. MWALIMU KUHUSU HUDUMA ZA MATIBABU KWA WATU WENYE ULEMAVU WASIO NA UWEZO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 17, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 17, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment