SAMIA – SERIKALI INALIPA MADENI YA BILIONI 900 KILA MWEZI




Wakati wananchi wakilalamikia fedha kutoweka mifukoni, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inatumia Sh900 bilioni kati ya Sh1.33 trilioni inazokusanya kila mwezi, kulipa madeni.

Alisema hayo wakati akifungua mkutano wa waganga wakuu wa mikoa na wilaya nchini mjini hapa jana.

Kauli yake imekuja wakati kukiwa na mjadala kuhusu uchumi, baadhi ya watu kusema hali inazidi kuwa mbaya wakati taasisi za Serikali zikitoa takwimu zinazoonyesha kuwa uchumi uko imara.

SAMIA – SERIKALI INALIPA MADENI YA BILIONI 900 KILA MWEZI SAMIA – SERIKALI INALIPA MADENI YA BILIONI 900 KILA MWEZI Reviewed by KUSAGANEWS on October 17, 2016 Rating: 5

No comments: