Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta ya Utalii mkoani Arusha unaotarajiwa kufanyika kesho.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa mkutano
kama huo utakaofanyika kesho ulifanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2012 hivyo
wameona ni vema serikali kushirikiana na wadau wa utalii kukaa pamoja kujadili
changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuboresha sekta hiyo.
Amesema kuwa mkoa wa Arusha ni
kitovu cha cha utalii na unachangia pato la mkoa kwa asilimia 20% na kitaifa
kwa asilimia 17%ambapo mwaka 2015 idadi ya watalii iliyoingia nchini ilikuwa
1,137,182 na kuingizia Taifa kiasi cha dola za kimarekani milioni 1.9 na kwamba
katika idadi hiyo asilimia 80%watalii walitembelea mkoa kwasababu ya
vivutio vingi vilivyopo mkoani humo.
Vilevile Gambo amesema kuwa katika mkutano huo wadau
mbalimbali watapata fursa ya kumuliza maswali waziri mwenye dhamana kwa upande
wa utalii ili kuondoa baadhi sintofahamu kwa baadhi ya maeneo kuhusu sekta ya
utalii kwa upande wa utalii.
”Wale wadau mbalimbali ambao watahitaji kuwa na maswali
pengine ya kupata majibu ya moja kwa moja kutoka kwa mhesahimiwa waziri
atakuwepo na amejidhatiti kutoa maelekezo vizuri ili kuondoa sintofahamu””
Pamoja na hayo ameongeza kuwa tarehe 27 septemba ni siku ya kusherekea
siku ya utalii duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema UTALII KWA WOTE na kwa mkoa wa arusha wameanza mapema ili
kujadili masuala mbalimbali ili ifikapo tarehe rasmi iwe ni siku ya kutoa
muelekeo wa hali ya utalii katika mkoa wa arusha na tanzania kwa ujumla.
WADAU WA UTALII KUKUTANA KESHO ARUSHA 22 SEPTEMBA KWENYE UKUMBI WA AICC
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 21, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 21, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment