ZIKIWA zimepita siku saba tangu kijana Saidi Mnyambi
(26) ang’atwe ulimi na jirani yake, Mwajabu Jumanne (36) hadi kupoteza uwezo wa
kuongea na kula, hatimaye Jeshi la Polisi limesema linawashikilia wote wawili
kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Peter Kakamba alisema mjini hapa jana kuwa polisi
imelazimika kuwashikilia wote wawili kutokana na maelezo yao kutofautiana.
Alisema wakati kijana huyo anadai kuwa tukio hilo lilitokea baada ya yeye
kulazimishwa kufanya mapenzi, mwanamke huyo naye anadai kuwa alimng’ata ulimi
wakati akijaribu kujiokoa ili asibakwe.
Kutokana na hali hiyo, Kamanda Kakamba alisema jeshi hilo limeona kuna haja ya
kuwashikilia wote wawili kwa uchunguzi zaidi ili kubaini ukweli wa jambo hilo
kabla ya kuwafikisha mbele ya Mahakama.
Mnyambi alinyofolewa theluthi moja ya ulimi wake na mke wa jirani yake kwa kile
kinachodaiwa kuwa ni kumlazimisha kufanya naye mapenzi Sikukuu ya Idd El Hajj saa
3.30 usiku.
Alidai kuwa siku ya tukio, mwanamke huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake
kwa kuwa alikuwa amelewa.
Hata hivyo, walipofika njiani inadaiwa kuwa mama huyo alimtaka kijana huyo
wafanye mapenzi jambo ambalo alimkatalia lakini akamwomba waagane, angalau kwa
kunyonyana ulimi (ampe denda), lakini ghafla kijana huyo alishtukia aking’atwa
ulimi na mama huyo na kukimbilia nyumbani kwake.
Muuguzi Mwandamizi Hospitali ya Mkoa wa Singida alikolazwa kijana huyo, Herman
Mallya amesema kuwa hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri ingawa hajapata
uwezo wa kuongea.
Alisema wakati kijana huyo anadai kuwa tukio hilo lilitokea baada ya yeye kulazimishwa kufanya mapenzi, mwanamke huyo naye anadai kuwa alimng’ata ulimi wakati akijaribu kujiokoa ili asibakwe.
Kutokana na hali hiyo, Kamanda Kakamba alisema jeshi hilo limeona kuna haja ya kuwashikilia wote wawili kwa uchunguzi zaidi ili kubaini ukweli wa jambo hilo kabla ya kuwafikisha mbele ya Mahakama.
Mnyambi alinyofolewa theluthi moja ya ulimi wake na mke wa jirani yake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kumlazimisha kufanya naye mapenzi Sikukuu ya Idd El Hajj saa 3.30 usiku.
Alidai kuwa siku ya tukio, mwanamke huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake kwa kuwa alikuwa amelewa.
Hata hivyo, walipofika njiani inadaiwa kuwa mama huyo alimtaka kijana huyo wafanye mapenzi jambo ambalo alimkatalia lakini akamwomba waagane, angalau kwa kunyonyana ulimi (ampe denda), lakini ghafla kijana huyo alishtukia aking’atwa ulimi na mama huyo na kukimbilia nyumbani kwake.
Muuguzi Mwandamizi Hospitali ya Mkoa wa Singida alikolazwa kijana huyo, Herman Mallya amesema kuwa hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri ingawa hajapata uwezo wa kuongea.
KIJANA ALIYENG'ATWA ULIMI NA JIRANI YAKE WATIWA MBARONI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 21, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 21, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment