Watu 11 wamefariki papo hapo na wengine 7 kujeruhiwa
baada ya basi la Super Shem lililokuwa likitokea Mbeya kwenda jijini Mwanza kugongana na daladala (Hiace) katika eneo la
Hungumalwa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
![]() |
| Haisi baada ya kupata ajali |
Diwani wa kata ya Hungumalwa, Shija Malando, amesema ajali hiyo imetokea leo
Septemba 21,2016 saa 12 asubuhi baada ya basi hilo kugongana uso kwa uso na
daladala iliyokuwa ikitokea kijiji cha Shilima wilayani Kwimba.
Diwani Malando amesema miili ya marehemu pamoja na majeruhi wamepelekwa hospitali ya Ngudu Kwimba na wengine hospitali ya wilaya Misungwi.
Diwani Malando amesema miili ya marehemu pamoja na majeruhi wamepelekwa hospitali ya Ngudu Kwimba na wengine hospitali ya wilaya Misungwi.
![]() |
| Basi la Super Shem baada ya kupata ajali |
Majeruhi wa ajali hiyo waliokuwa kwenye basi wamesema basi lao lilikuwa kwenye
mwendo mkali na lilipofika eneo la tukio ghafla daladala hiyo iliingia
barabarani na hivyo dereva wa basi kushindwa kuikwepa.
Inaelezwa kuwa waliopoteza maisha na kujeruhiwa ni abiria waliokuwa kwenye daladala.
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limethibitisha kutokea kwa
tukio hilo.
BASI LA SUPER SHEM LAGONGANA NA HIACE NA KUUA WATU 11 HUNGUMALWA KWIMBA MWANZA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 21, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 21, 2016
Rating:



No comments:
Post a Comment