WATUMBULIWA KWA KUSABABAISHA HASARA YA SHILINGI MILIONI MBILI KATIKA KITUO CHA AFYA CHA KALOLENI ARUSHA
![]() |
| Mkurugenzi wa jiji la Arusha Bw Athumani Juma Kihamia |
Mkurugenzi wa
Jiji la Arusha Bwana Athumani Kihamia amewasimamisha kazi watumishi wawili wa
Idara ya Afya kutoka Kituo cha Afya Kaloleni ambao ni Mfamasia Zephania Ntaturu
na msimamizi wa maabara Joyce Kitinye kwa kosa la upotevu wa Dawa na
Vitendanishi vyenye thamani ya shilingi milioni 2.
Mkurugenzi
Kihamia amefikia uamuzi huo mara baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watu
mbalimbali na hatimaye kufanya kikao kilichojumuisha Mganga mkuu wa Jiji na
Uongozi wa Kituo cha Afya Cha Kaloleni.
Katika Kikao
hicho watuhumiwa walikiri kuhusika na upotevu wa dawa na vitendanishi hivyo na
kuomba kurejesha fedha mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu; zenye dhamani ya
vifaa na dawa zilizopotea jambo ambalo mkurugenzi Kihamia hakukubaliana
nalo;kwa kuwa suala hilo ni wizi wa mali ya umma.
Aidha
Mkurugenzi wa Jiji amewataka Watumishi wote kutekeleza majukumu yao kwa
kuzingatia kanuni, sheria na taratibu za Utumishi wa Umma; na kuonya kwamba
hakuna mtumishi atakayebaki salama kwa kwenda kinyume na miiko ya utumishi wa
Umma.
Pia Mkurugenzi
amemwagiza Mkaguzi wa ndani kufanya ukaguzi katika vituo vya afya na zahanati
zilizopo katika Halmashauri ya Jiji la Arusha; ili kujua kama kuna wizi wa dawa
na vifaa ama la.
WATUMBULIWA KWA KUSABABAISHA HASARA YA SHILINGI MILIONI MBILI KATIKA KITUO CHA AFYA CHA KALOLENI ARUSHA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 19, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 19, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment