![]() |
| Mkuu wa wilaya ya arusha Mjini Bwana Gabriel Fabian Daqaro |
Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Fabian Daqaro
amewataka watumishi wa serikali kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii ili
kutatua kero za wananchi zinazowasumbua katika maeneo yao kwenye maeneo yao.
Daqaro amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa
serikali katika halmashauri ya jiji la arusha na kusema kuwa kuna baadhi ya
watumishi wa serikali wamekuwa wakijifanya kama Mungu watu kwa kutoa maneno ya
kashfa kwa wananchi pamoja kushindwa kutatua kero zinazowakumba wananchi.
Pia mewataka watumishi wa serikali kuwatendea haki wananchi
Pia mewataka watumishi wa serikali kuwatendea haki wananchi
Wanapohitaji huduma pidi wanapofika katika ofisi zao na
wasiwanyanyase kwa wananchi ndiyo wateja namba moja na ndiyo wamemchagua raisi
wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe magufuli.
Kwa upande wake Mkurugenz wa jiji la arusha Athumani kihamia amesema kuwa watumishi wanalipwa mshahara kila mwezi hivyo hawezi mvumilia mtendaji yeyote katika kitengo chochote cha halmashauri anaenda kinyume na taratibu na kushindwa kuhudumia wananchi na kutatua kero zao.
![]() |
| Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Juma kihamia akiwa ameshika kipaza sauti |
Pamoja na hayo Kihamia amesema kuwa kuna baadhi ya watumishi
wa serikali wanawanyanyasa wananchi na wakati mwingine mpaka waandishi wa
habari ambao wanawasaidia kutoa taarifa ambazo jamii inatakiwa izitambue jambo
ambalo amesema hatovumilia watumishi wenye tabia hizo za unyanyasaji.
WATUMISHI WA SERIKALI ARUSHA MSIWE KAMA MIUNGU WATU TATUENI KERO ZA WANANCHI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 17, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 17, 2016
Rating:



No comments:
Post a Comment