Ofisi ya UVCCM mkoa wa Arusha yapigwa mnyororo mwenyekiti wa umoja huo Ole Sabaya asema waliofunga ni vibaka avunja kofuli na kufungua ofisi hiyo.
Akizungumza nje ya ofisi hiyo Mwenyekiti Wa Uvccm mkoa Martin Ole Sabaya amesema waliofunga ofisi ni vibaka na hawatambui hivyo alisema ofisi yake haiwezi kuingiliwa ovyo.
" Hawa waliofunga ofisi ni vibaka tena waizi wakubwa hatujakaa tukatafakari mali zilizopotea ndani ya ofisi ili kubaini na wachache waliofanya hivi tumeshawajua" alisema Ole Sabaya.
Alisema hakuna Katibu anateruhusiwa kuingia hapo aliyeripoti na aliyekuwepo hakuna anayeruhusiwa bali hadi baraza litakapo kaa ndipo maamuzi yatakapo tolewa.
Mwenyekiti huyo alisema wapo watu ambao ni wanachama lakini wanakihujumu chama hivyo hawezi kukubaliana na hilo.
Alisema wasiompenda waombe Mungu awahi kumaliza uongozi wake mapema kwani yeye hawezi kuhamishwa kama makatibu hivyo atapambana kuhakikisha maslahi ya chama yanaonekana.
Ofisi hiyo ilifungwa alfajiri Jana majira ya saa 10 ambapo walikuja kikundi cha watu wakaanza kupambana na askari waliokuwa wakilinda eneo hilo kwa kuwatupia mawe na hatimaye wakafanikiwa kuweka kofuli yao.
Baada ya muda alifika mwenyekiti huyo na kuvunja kofuli hiyo na kufanikiwa kufungua mlango huku akidai kuwa hayuko tayari kuona waizi wakifunga ofisi yake ambapo alisema ameshampigia katibu wa umoja huo kuwa asiingie katika ofisi hiyo hadi baraza litakapo kaa siku ya jumamosi kufanya maamuzi.
Awali kabla ya tukio la kufunga ofisi kutokea Katibu wa umoja huo Ezekiel Mollel inasemekana kuwa alishapewa barua ya uhamisho kutakiwa kuhama mkoa huo jambo ambalo limeleta mkinzano baina ya uongozi wa umoja huo.
Akizungumza na Gumzo Tz juzi ofisini kwake Katibu huyo alipotembelewa na mwandishi wa habari hizi juu ya jambo hilo alisema ni kweli barua ilishakuja kua anatakiwa kuhama na tayari alishakuja mtu kuripoti ila kamati ya utekelezaji ilimtaka kufanya taratibu za kutekeleza majukumu ya makabidhiano ya ofisi ili aweze kukabidhi ofisi hiyo.
Hata hivyo Mollel alisema kutokana na miradi ya umoja huo kuhujumiwa yeye amejipanga kusimamia miradi hiyo ili kuweza kuingiza pato katika chama jambo ambalo alisema anapigwa vita.
"Haiwezekani maduka ya Chama ya biashara watu wanalipa sh. 5000 kwa mwezi hapa mjini huku watu wachache wakifaidi mamilioni ya pesa na sisi kupata kiasi kidogo namna hii hiyo nitaipiga vita na ninajua kuna kikundi cha watu wachache wanatafuta kuniondoa ili waendelee kula" alisema Mollel.
Alisema lengo lake siyo kung' ang' ania ofisi bali anatetea maslahi ya vijana yasiendelee kuwa mikononi mwa watu wachache.
Kufuatia mgogoro huo kada wa chama hicho Amoni Filemoni ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi.
HAKUNA ATAKAEFUNGUA OFISI ASEMA MWENYEKITI UVCCM ARUSHA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 15, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 15, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment