MAFANIKIO YA MKURUGENZI WA ARUSHA ,MKUU WA MKOA NA ,MKUU WA WILAYA,KWA WALIMU YAONEKANA BAADA YA KUTATUA TATIZO LA MADENI YA WALIMU 701 WALIOKUWA WANADAI SERIKALI KIASI CHA SH MILIONI 169.8
Jumla
ya shilingi 169.8 milioni wameapatiwa waalimu 701wa shule za msingi na
sekondari kutoka kwenye fedha ambazo zilitakiwa kulipa posho za nauli na simu
za madiwani wa jiji la Arusha.
Akiongea na wanahabari
ofisini kwake jijini hapa mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro
alisema kuwa kutokana na malimbikizo ya fedha za likizo,kufiwa,nauli, uhamisho
waliokuwa wanadai walimu ndio maana tumeamua kuwalipa ili waweze kufanyakazi ya
kufundisha watoto wetu kwa moyo.
Daqqaro alisema kuwa
baada ya kikao na mkuu wa mkoa Mrisho Gambo na waalimu wa shule 48 za jiji la
Arusha, na kuagizwa kuhakikisha walimu wanalipwa stahiki zao ndani ya wiki
mbili na agizo hilo tumelitiza na walimu wamelipwa fedha zao.
Alisema kuwa fedha
zilizolipwa waalimu hao tumezitoa kwenye fedha zilizokuwa wakijilipa madiwani
posho za usafiri na posho za simu na kuzielekeza fedha hizo kutatua kero ya
waalimu na mwisho wa siku vijana wetu wapate elimu stahiki bila manung'unuko kutoka
kwa waalimu.
''Hapa napenda
tusiingize ushabiki wa kisiasa katika hili na tuache kuzusha maneno maneno
yanayaashiria uvunjifu wa amani kama kweli fedha hizo wanadai walifuta iwaje
leo waendeleze maneno''alisema DC Daqqaro.
Alisema kuwa serikali ya
awamu ya tano ipo kuhakikisha wananchi walio wengi wanaondolewa kero zao kwa
wakati na kuondosha kabisa kero mbali mbali ndani ya jamii ikiwemo waalimu
kupewa stahiki zao kwa wakati.
Akawataka waalimu hao
kuhakikisha malengo ya mkoa kuongeza ufaulu yamefikiwa kwa kufanyakazi kwa moyo
huku serikali ikiendelea kumalizia malalamiko mbali mbali ya waalimu wa mkoa
wetu.
Malipo hayo ya waalimu
701 yametokana na agizo la mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwataka dc na
mkurugenzi wa jiji la Arusha Athman kihamia kuhakikisha malalamiko ya waalimu
walioyatoa kwenye mkutano wao yanatekelezwa ndani ya wiki mbili .
MAFANIKIO YA MKURUGENZI WA ARUSHA ,MKUU WA MKOA NA ,MKUU WA WILAYA,KWA WALIMU YAONEKANA BAADA YA KUTATUA TATIZO LA MADENI YA WALIMU 701 WALIOKUWA WANADAI SERIKALI KIASI CHA SH MILIONI 169.8
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 25, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 25, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment