Serikali imesema kuwa inaanza kufanya maboresho kwa kuandaa na kuhakikisha Sera ya Uboreshaji wa Viwanda vya Dawa vilivyopo nchini kwa kuwawezesha na kuwajengea uwezo wenye viwanda nchini ili waweze kuzalisha dawa na kupunguza uagizaji wa dawa kutoka nje ya nchi.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo
kwa niaba ya Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,
Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza katika Kongamano la 49 la Chama Cha
Wafamasia Tanzania (PST),linalofanyika jijini hapa kwa siku mbili.
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Mashaka Gambo akitoa hotuba katika ufunguzi wa kongamano la 49 la Chama cha Wafamasia Tanzania
|
Akizungumza
kwa niaba ya Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,alisema kuwa kutokana
na umuhimu wa sekta hiyo ya dawa, Serikali inaangalia taaluma hiyo kwa macho
mawili kwa lengo la kuiboresha ili iweze kutoa huduma bora.
"Wizara
yangu inaangalia taaluma hii kwa macho mawili katika kuhakikisha kuwa sekta ya
dawa inaboreka na inakua na hatimaye kuweza kukuza uchumi wetu, kwa kuwawezesha
na kuwajengea uwezo wenye viwanda nchini ili waweze kuzalisha zaidi ikiwa ni
pamoja na kuwahakikishia soko ndani ya nchi na kupunguza uagizaji wa dawa
kutoka nje ya nchi na hivyo kuwa na dawa bora, salama na zenye ufanisi"
"Endapo
tutazalisha dawa zetu wenyewe hii itatupunguzia gharama zisizo za lazima
kuagiza dawa nje ya nchi, sambamba na hili pia tunaboresha vyuo vya Wafamasia
ili waweze kutoka wataalamu bora wa masuala haya ya madawa,”alisema Gambo
|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho
Gambo(Kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na dawa Hiti
Silo katika Kongamano la wafamasia linalofanyika katika Jiji la Arusha.
|
"Mbali
na changamoto ya upungufu wa dawa, wafanyakazi wasio waadilifu ambao wanatumia
nafasi zao vibaya wanashirikiana na baadhi ya wafanyabiashara na kuuza
dawa, hili ni suala muhimu PST jadilianeni suala la maadili kwani hatua za
kisheria dhidi yao zitachukuliwa"alisema
|
Wanachama wa PST wakifuatilia ufunguzi
wa Kongamano
|
Awali
Rais wa PST, Michael Kishiwa, aliiomba Serikali kuongeza udahili wa wanafunzi
wa famasia wakiwemo mafamasia wasaidizi ili kutoa dawa sahihi kwa wagonjwa.
Alisema
hivi sasa idadi ya watanzania ni kubwa, lakini wataalamu wa dawa Wafamasia ni
1,200, hali inayochangia kuwepo kwa watoa huduma hiyo wasio na sifa.
Alisema
kutokana na kukosekana wanataaluma kumekuwepo na changamoto kubwa ya baadhi yao
kukiuka maadili na wengine kufanya kazi ya utoaji dawa pasipokuwa na uelewa
nayo, hali ambayo hatari kwa afya za binadamu.
“Tunashirikiana
na baraza la usajili la wafamasia katika kukemea vitendo hivyo vya ukiukwaji wa
maadili na ndiyo maana tunaiomba serikali iongeze udahili na vyuo vinavyotoa
taaluma hii"alisema
|
Wajumbe wa kongamano wakiendelea
kufuatilia Hotuba ya Ufunguzi
|
Naye
Msajili wa Baraza la Wafamasia, Elizabeth Shekalage alisema kwa sasa wananchi
wengi wamechukulia huduma ya dawa ni biashara na kuwa baraza limejipanga
kupambana na watu wanaofanya huduma hiyo ni biashara huku wakikiuka
maadili.
"Uchache
wa wanataaluma unasababisha kika mtu aone hii ni biashara huria na yeyote
anaweza kuifanya,kuna uhaba mkubwa wa fundi dawa sanifu,mafundi dawa
wasaidizi,dawa ni sumu hivyo tunasimamia hili ili kuepusha madhara kwa
watumiaji"alisema Elizabeth
Kongamano
la Mwaka huu linaenda na kauli mbiu isemayo kuelezea ubora,usalama,ufanisi na
upatikanaji wa huduma bora za kifamasia.
SERIKALI KUANZA MKAKATI WA KUFANYA MABORESHO YA UPATIKANAJI WA DAWA KWA UPANDE WA AFYA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 30, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment