Daktari ampiga ngumi mgonjwa na kumuua

 Kanda ya video ya CCTV imetolewa ambapo daktari mmoja nchini Urusi alimpiga ngumi mgonjwa na kumuua
 
Kisa hicho kilitokea katika mji wa Belgorod kilomita 670 kusini mwa mji mkuu wa Moscow mnamo mwezi Disemba tarehe 29.

Mgonjwa huyo alikuwa amempiga teke muuguzi mmoja kabla ya daktari huyo kumpiga ngumi ya kichwa kulingana na vyombo vya habari vya Urusi na kuzirai kabla ya kuaga dunia akiwa hospitalini.

Wachunguzi wanadhani kwamba hakumuua kwa makusudi lakini wameanzisha kesi ya uhalifu.
Habari hiyo ilisambaa baada ya kanda hiyo kutolewa.

BBC 
Daktari ampiga ngumi mgonjwa na kumuua Daktari ampiga ngumi mgonjwa na kumuua Reviewed by KUSAGANEWS on January 12, 2016 Rating: 5

No comments: