Moja ya ahadi kubwa alizoziweka Rais Magufuli tangu ameanza kazi na Serikali yake ya awamu ya tano iko ya kubana matumizi na kukabiliana na ubadhirifu.
Taarifa nyingine imenifikia kutoka Ikulu kuhusu maamuzi ya Rais Magufuli, kaamua kufanya maamuzi mengine kusimamisha watumishi watano, tuhuma zinaziwakabili ni matumizi mabaya ya pesa Serikali.
Waliosimamisha ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA, Dickson Maimu pamoja na wengine wanne ambao wanafanyiwa uchunguzi.
Wafanyakazi wanaofanyiwa uchunguzi ni hawa;
Joseph Makani– Mkurugenzi wa TEHAMA
Rahel Mapande– Afisa Ugavi Mkuu
Sabrina Nyoni– Mkurugenzi wa Sheria
George Ntalima– Afisa Usafirishaji
Rais Magufuli kawasimamisha wengine watano leo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha..
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 25, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 25, 2016
Rating:



No comments:
Post a Comment