Simba wa milimani aliyeuawa katika
jimbo la Idaho, nchini Marekani ameshangaza wengi kutokana na hali
kwamba alikuwa na meno ya ziada kichwani.
Simba huyo aliuawa na wawindaji walioidhinishwa tarehe 30 Desemba.
Idara ya Wanyamapori na Samaki ya Idaho imesema meno hayo huenda ni masalio ya pacha ambaye labda alifariki akiwa tumboni, au labda inatokana na saratani.
Wataalamu wa vimbe katika jimbo hilo wanasema hawajawahi kuona ulemavu wa aina hiyo awali.
Simba huyo aliwindwa na kuuawa baada ya kumshambulia mbwa karibu na mji wa Weston. Mbwa huyo alinusurika lakini mwindaji akatumwa kumuwinda simba huyo na kumuua.
Afisa wa uhifadhi wa wanyama alikagua mzoga wa simba huyo kama ilivyo sheria na ndipo akagundua meno hayo.
Mnyama huyo pia alikuwa na masharubu kwenye paji la uso kushoto
Simba wa kushangaza aliyeuawa Marekani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 12, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 12, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment