Mwenyekiti Mtendaji wa
IPP Dr Reginald Mengi amesema Maendeleo ya Watanzania hayataletwa na watu wa
nje, bali yataletwa na Watanzania wenyewe kwa kutumia juhudi na umoja wao.
Mwenyekiti Mtendaji wa
IPP Dr Reginald Mengi ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizindua
rasmi uuzwaji wa hisa za Asasi ya kifedha ya YETU Microfinance P.L.C, ambapo
alinunua hisa 40,000 zenye thamani ya shilingi milioni 20, ili kudhuhirishia
imani yake kwa asasi hiyo iliyoasisiwa na Watanzania.
Dr Mengi pia
amewahamasisha wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kununua hisa za asasi hiyo,
na kuwataka wajibidishe katika kuusaka ujajiri kwa njia zinazompendeza
Mwenyezimungu.
Mapema Mkurugenzi wa
Yetu Microfinance P.L.C Bw. Altemius Millinga alisema asasi ya
fedha ya Yetu Microfinance P.L.C imepata kibali kutoka Mamlaka ya Masoko
ya Mitaji na Dhamana, cha kuuza hisa zipatazo milioni 25 kwa shilingi
500 kila moja, katika kipindi cha kati ya Juni 18, 2015 na Julai 30,
2015. Kwa sababu hiyo amewahimiza wajasiriamali kuchangamkia hisa hizo, ambapo
kima cha chini cha ununuzi ni ni hisa 200 zenye thamani ya shilingi laki
moja.
Wakati wa uzinduzi huo
wajasiriamali wawili Bi. Johari Mkonde na Bi Lucia Kimamba walitoa
ushuhuda wa jinsi walivyofanikiwa katika ujasiriamali wao
Watanzania washauriwa kutumia juhudi na umoja kujiletea maendeleo.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 23, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment