Rwanda imeshutumu uamuzi wa mamlaka za Uingereza
kumkamata kiongozi wake wa ujasusi wa Rwanda, Karenzi Karake, ambaye anatakiwa
Uhispania kwa madai ya uhalifu wa kivita.
Waziri wa maswala ya kigeni Louis Mushikwabo ameelezea
hatua hiyo kama wazimu na lengo lake ni kukandamiza waafrika akiongezea kwamba
inatokana na madai ya watu wanaotaka kuwanyima haki waathiriwa wa mauaji ya
kimbari nchini humo mwaka 1994.
Mamlaka ya Uhispania inataka kumhoji bwana Karake
kuhusu kuhusika kwake katika mauaji ya raia wakiwemo wafanyikazi wa msaada
kutoka Uhispania baada ya mauaji hayo.
Kesi ya Uhispania ilianzishwa mwaka 2008,lakini
waandishi wanasema kuna wasiwasi kuhusu ushahidi wa mashtaka.
Makumi ya maelfu ya raia wa Rwanda wanadaiwa kufariki
baada ya mauaji hayo ya kimbari aidha kupitia mauaji ya kulipiza kisasi nchini
Rwanda ama katika kile waandishi wanataja kama wimbi la mauaji ya kikabila
katika taifa jirani la jamhuri ya kidemokrasia ya Congo baada ya wapiganaji
wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda kuwalazimisha raia wa kabila la Hutu
kutoka katika kambi za wakimbizi karibu na mpaka.
Takriban watu laki nane hususan wale wa kabila la
Tutsi waliuawa na wenzao wa kabila la Hutu katika mauaji ya kimbari yaliochukua
miezi mitatu.
Rwanda yashtumu kukamatwa kwa afisa wake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 23, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment