Mwalimu mmoja mkuu amekiri kufanya ngono na wavulana
wawili wenye umri mdogo.
Anne Lakey, mwenye umri wa miaka
55, kutoka eneo la Stanley, katika kaunti ya Durham, amekanusha makosa 13 dhidi
yake ya kufanya matendo ya aibu kwa kushikashika sehemu za siri wavulana wawili
miaka ya themanini.
Lakini jaji katika mahakama ya
Teesside Crown, alimpata na hatia ya makosa hayo yote baada ya kesi iliyochukua
majuma mawili.
Mahakama ilisikiza ushahidi wa
namna alivyokuwa akitenda matendo hayo ya kuudhi na aibu katika kipindi cha
miaka mitatu mfululizo.
Atahukumiwa jela Jumatano wiki
hii.
Mahakama iliambiwa kuwa baadhi ya
makosa yalifanyika pale Lakey alipokuwa mwalimu wa kufundisha somo la historia
akiwa na umri wa miaka 20.
Lakey, ametajwa na waendesha
mashtaka kama "mnyama wa ngono", alimlenga mvulana wa miaka 15 na
waathiriwa wengine wawili wenye umri wa kati ya miaka 13 au 14.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi
hiyo, mmoja wa waathiriwa aliwaambia majaji kuwa mama huyo wa mtoto mmoja
alimuondolea ubikra pale alipomtaka amtizame alipokuwa akioga.
Lakey alifanya kazi yake ya
ualimu kwa ushindi mkubwa kwani alisifiwa mno kwa kufaulisha Shule hiyo
iliyokuwa imedorora kielimu na kuifanya mojawepo ya shule iliyopata mafanikio
makubwa.
Lakini mnamo mwaka 2012, mojawepo
wa waathiriwa alituma ujumbe kwa njia ya barua pepe hadi shuleni humo,
iliyosababishwa afutwe kazi na kisha polisi wakafahamishwa.
Mwalimu mkuu ashiriki ngono na wanafunzi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 23, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment