Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akimvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Mhitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili ambaye amefanya vizuri kwa upande wa Gwaride, Stafu Sajini Boniphace Felix. Mhitimu huyo amevishwa cheo hicho kwa niaba ya Wahitimu 216 wa Mafunzo hayo. Maafisa wa Jeshi la Magereza wakionyesha umahiri mkubwa wa mbinu mbalimbali za kujihami na adui kama wanavyoonekana kikakamavu katika picha wakati wa hafla fupi ya kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili. Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili kwa Maafisa wa Jeshi la Magereza. Kikundi cha kwaya kinachoundwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza wa Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga kikitumbuza mbele ya Mgeni rasmi, IGP Ernest Mangu(hayupo pichani)katika sherehe za kufunga Mafunzo hayo ya Uongozi Daraja la Pili, Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga. Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini matukio mbalimbali katika sherehe hizo za kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Erasmus Kundy(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza). Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili ambayo yamefungwa rasmi leo Juni 22, 2015 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam. Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili wakipita mbele ya Mgeni rasmi IGP Ernest Mangu(hayupo pichani) katika mwendo wa haraka wakitoa heshima leo Juni 22, 2015 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga. Jumla ya Wahitimu 216 wamehitimu Mafunzo Uongozi Daraja la Pili na kupandishwa cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza. Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu akipokea Salaam ya heshima kutoka kwa Gwaride lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili(kushoto katika Jukwaa) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja. Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akifurahia onesho Maalum la Maafisa wa Jeshi la Magereza kutoka Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani(katikati) ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu(kushoto) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile wakifurahia onesho hilo kama wanavyoonekana katika picha.
No comments:
Post a Comment