ALI KIBA AWEKA WAZI KUHUSIANA NA BIFU NA DIAMOND PLUTNUMZ, AZUNGUMZIA KUHUSU TeamDiamond Na TeamKiba.




Staa wa Bongo Fleva,Ali Kiba amefunguka kuwa hana ugomvi na msanii mwenzake,Diamond Platinumz kama ambavyo mashabiki wanadhani na hafurahishwi na timu za mashabiki zinazojiita ‘TeamDiamond na TeamKiba’ambazo zipo kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram lakini hawezi kuwazuia.

Akizungumza na Leo Tena ya Clouds Fm,alisema kuwa wao ni vioo vya jamii na wanapendwa na watu wengi na anapoona yanatokea mambo hayo kwenye  mitandao hiyo ya kijamii hawezi kufanya chochote na kuwaingilia mashabiki hao.


‘’Kiukweli sifurahishwi na timu hizi na naona kinachoendelea kwenye mitandao lakini siwezi kufanya chochote na kuwaingilia mashabiki,ila ushauri wangu ni bora wangeacha tu,’Amesema Kiba.
Pia amesema yeye na Diamond huwa hawashirikiani, lakini kwa upande wa timu zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii hawezi kuwazuia kwa sababu hana nguvu hiyo kwa sababu hawajui ni kina nani.
ALI KIBA AWEKA WAZI KUHUSIANA NA BIFU NA DIAMOND PLUTNUMZ, AZUNGUMZIA KUHUSU TeamDiamond Na TeamKiba. ALI KIBA AWEKA WAZI KUHUSIANA NA BIFU NA DIAMOND PLUTNUMZ, AZUNGUMZIA KUHUSU TeamDiamond Na TeamKiba. Reviewed by KUSAGANEWS on June 23, 2015 Rating: 5

No comments: