Kocha mkuu wa Timu ya Taifa Stars afukuzwa kazi

Kamati ya utendaji ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imesitisha ajira ya kocha mkuu wa timu ya taifa TAIFA STARS, MAART NOOIJ kuanzia leo kufuatia kufanya vibaya kwa timu hiyo katika michezo yake ya karibuni. 

Maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha kamati hiyo ya utendaji ya TFF kilichokutana jana kisiwani UNGUJA ZANZIBAR. 

Kulingana na taarifa iliyotolewa na afisa habari wa TFF –BARAKA KIZUGUTO, inasema kamati ya utendaji imefikia hatua hiyo kutokana na matokeo mabaya ya TAIFA STARS ikiwemo kipigo cha jana cha magoli MATATU kwa BILA kutoka kwa timu ya taifa ya UGANDA katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa bingwa barani AFRIKA-CHAN. 

Pia kamati hiyo ya utendaji ya TFF imelivunja benchi lote la ufundi la TAIFA STARS kuanzia leo. 

Habari zaidi zinaarifu kuwa timu ya TAIFA kwa sasa itakuwa chini ya kocha CHARLES MKWASA akisaidizi na SELEMAN MATOLA. 

MKWASA ni kocha msaidizi wa YANGA huku MATOLA akiwa kocha msaidizi wa SIMBA.
Kocha mkuu wa Timu ya Taifa Stars afukuzwa kazi Kocha mkuu wa Timu ya Taifa Stars afukuzwa kazi Reviewed by KUSAGANEWS on June 22, 2015 Rating: 5

No comments: