Kombe la FIFA kwa wanawake hatua ya mtoano yaanza



fainali za kombe la FIFA la dunia kwa wanawake zinazoendelea nchini CANADA ambapo michezo ya hatua ya mtoano ya 16 bora inafanyika kwa sasa. 

Katika michezo iliyochezwa mwishoni mwa juma wawakilishi pekee wa AFRIKA waliosalia katika fainali hizo CAMEROON wamesukumizwa nje baada ya kula mweleka wa goli MOJA kwa BILA dhidi ya CHINA, huku AUSTRALIA, UFARANSA na wenyeji wa CANADA wakiungana na CHINA kusonga mbele katika hatua ya robo fainali. 

Bao pekee lililofungwa dakika ya 80 ya mchezo na KYAH SIMON limetosha kuwapa ushindi wa goli MOJA kwa BILA kinadada wa AUTSRALIA dhidi ya BRAZIL na kuwavusha katika hatua ya robo fainali. 

Katika matokeo mengine nyota wa UFARANSA, MARIE LAURE DELIE alifunga magoli MAWILI huku bao lingine likifungwa na ELO DIE THOMIS na kuwapa UFARANSA ushindi wa magoli MATATU kwa BILA dhidi ya KOREA KUSINI na hivyo kufuzu kwa hatua ya robo fainali. 

Wenyeji CANADA nao wamepata ushindi wa goli MOJA kwa BILA dhidi ya SWITZELAND na kufuzu hatua ya robo fainali. 

Leo inachezwa michezo mingine miwili kuwania kufuzu kwa hatua hiyo ya robo fainali ambapo bingwa wa zamani wa dunia NORWAY wakiwa na ukame wa miaka 20 wa taji hilo wanachuana na ENGLAND huku mabingwa mara mbili wa taji hilo MAREKANI wakicheza dhidi ya COLOMBIA. 

KESHO ni zamu ya JAPAN dhidi ya UHOLANZI.

Kombe la FIFA kwa wanawake hatua ya mtoano yaanza Kombe la FIFA kwa wanawake hatua ya mtoano yaanza Reviewed by KUSAGANEWS on June 22, 2015 Rating: 5

No comments: