Jirani zetu Kenya ambao wamebadilisha vyama vya kuongoza serikali zaidi ya mara 2 wanaonekana kupiga hatua kubwa tu ya kimaendeleo.Bajeti ya Kenya iliyopitishwa inaonyesha kushusha ushuru na kodi kwenye bidhaa muhimu kwa ajili ya kuwawekea unafuu wa maisha wananchi wake huku ikiwekeza sana kwenye ukusanyaji wa fedha za kigeni.

Pamoja na kwamba Tanzania tunawazidi rasilimali Kenya lakini bado nchi ya Kenya imetenga bajeti ya mwaka 2015/2016 kiasi cha trilioni 47 kwa ajili ya maendeleo ya Elimu,Barabara,Kilimo,Afya n.k, huku ikiwa ina idadi ya watu milioni 38.Wakati huo huo,Tanzania imetenga bajeti ya mwaka 2015/2016 kiasi cha trilioni 22.5 kwa ajili ya uchaguzi mkuu na maendeleo huku idadi ya watanzania ikionyesha kuwa inakaribia milioni 50.

 Watia nia wa Urais ndani ya CCM kwa ajili ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi October ambao wengi wao ni mawaziri na wengine walijiuzuru kwa kashfa, wanasema watainua uchumi wa taifa wakati huo wameshindwa kuinua uchumi wa Taifa hili la Tanzania wakiwa kama mawaziri na watendaji wakuu wa serikali ya CCM.

Maendeleo ya Taifa hili hayawezi kuja kwa watu wa chama cha siasa kile kile,watu wale wale,wenye akili zile zile na wenye kufanya kazi kwa mazoea yale yale chini ya mfumo ule ule.Hakuna mtanzania mwenye hisa ndani ya CCM na kuna haja kubwa tu ya kufanya mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Ni aibu kwa taifa lililojitawala kwa zaidi ya miaka 50 hadi toilet paper inatoka China huku vijana tukijibizana kwa majina ya timu Membe,mara team Lowassa,team Wasira n.k wakati huo hakuna hata kitu kilichotengenezwa Tanzania ambacho tunaweza kujivunia kuanzia mavazi yetu chini mpaka juu.Hivi utapaje ajira wakati hata nguo za ndani tu tunazovaa zinatengenezwa 

China huku tukiwapigia chapuo watia nia wa CCM waliokaa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 na kuuwa viwanda vyotee?

 
Reviewed by KUSAGANEWS on June 18, 2015 Rating: 5

No comments: