Shirika lisilo la
Kiserikali la Oxfam hapo jana lilikabidhi vituo vya kusindika maziwa
kwa wanawake wa vikundi vinne kutoka vijiji vya Engaresero, Pinyinyi, Malambo na Piyaya vilivyoko katika wilaya ya Ngorongoro.
Akipokeavituo hivyo kwa
niaba ya wanavikundi hao, Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro
John Kulwa Mgalula, alisema ana imani vituo hivi vitawasaidia wanawake kukua
kiuchumi na kuepuka kuwa tegemezi kwani wanawake wengi wamekuwa na sifa ya
uvumilivu,
uangalifu wa hali ya juu na kwamba mara nyingi wao hufanya vitu kwa uaminifu.
Mkurugenzi aliyashukuru
mashirika ya Oxfam waliofadhili ujenzi wa vituo hivi pamoja na PALISEP
waliotekeleza mradi huu kwa jitihada mbalimbali ambazo yamekuwa yakifanya
katika wilaya ya Ngorongoro ili kuwakuza wanawake kiuchumi huku akitaja miradi
mingine iliyofadhiliwa na Oxfam kuwa ni pamoja na ujenzi wa maghala ya
kuhifadhia chakula, ujenzi wa majosho, pamoja na ujenzi wa vyanzo vya maji.
Akikabidhi vituo hivyo,
Stellah Julius kutoka Oxfam alisema, “Baada ya kufanya utafiti
uliowashirikisha wanawake wa vijiji hivi vinne walituambia kwamba wanahitaji
vituo vya kusindika na kuhifadhia maziwa. Tumewajengea vituo hivi mvitumie kwa
maendeleo yenu.” Stellah pia aliipongeza serikali na wadau mbalimbali kwa kutoa
ushirikano mkubwa uliopelekea kufanikisha ujenzi wa vituo hivyo ikiwemo kutoa
maeneo
ya ardhi ya vijiji hivyo vinne.
Aidha Stellah aliwataka
wanavikundi hao kuwa wabunifu wa namna ya kujiendeleza
kibiashara na kuepuka kutegemea mashirika na taasisi ambazo zipo kwa muda tu.
Naye Mkurugenzi wa
shirika la PALISEP Robert Kamakia alisema shirika lake limewajengea
uwezo wana vikundi hao kwa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na mbinu mbalimbali
za kibiashara pamoja na kuwafundisha namna za kutunza maziwa kwa usafi.
Kwa upande wake Thomas
Nade, Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ngorongoro
aliwataka wanavikundi hao kusajili vikundi vyao mapema ili vitambulike kisheria
na waweze kunufaika kwa namna mbalimbali ikiwemo kupatiwa mikopo na kufungua
akaunti ya benki
Wanawake kutoka vijiji
hivi vinne wanatarajia kunufaika kwa kujipatia kipato kutokana na
kuuza maziwa na siagi.
Akionyesha furaha yake,
Mariam Lembilika kutoka kijiji cha Malambo alisema, “Mimi kama
mwanamke ambaye nina watoto watano na sina mume natarajia kutumia kipato
kutokana na biashara hii kusomesha watoto.
Naye Mary Saigulan kutoka kijiji cha Engaresero alisema,
“Tutauza maziwa na siagi na kujipatia fedha nyingi ambazo zitatusaidia
kuanzisha miradi mingine na kutuwezesha kujitegemea“
Ujenzi wa vituo hivi vinne umegharimu takribani
shilingi za kitanzania milioni
120 na kila kimoja kina jokofu linalotumia umeme wa jua, mashine za
kusindika maziwa, madumu ya kuhifadhia maziwa, vipima joto, vipimo vya kupimia
ubora wa maziwa, tenki la maji pamoja na mashimo mawili ya vyoo na bafu.
Vikundi hivyo vya NOSOTWA
(Engaresero), NAPONU (Pinyinyi), NYUWAT (Malambo) na NASERIYAN (Piyaya) vina
wana kikundi wapatao 30 kila kimoja
kwa wanawake wa vikundi vinne kutoka vijiji vya Engaresero, Pinyinyi, Malambo na Piyaya vilivyoko katika wilaya ya Ngorongoro.
kiuchumi na kuepuka kuwa tegemezi kwani wanawake wengi wamekuwa na sifa ya uvumilivu,
uangalifu wa hali ya juu na kwamba mara nyingi wao hufanya vitu kwa uaminifu.
waliotekeleza mradi huu kwa jitihada mbalimbali ambazo yamekuwa yakifanya
katika wilaya ya Ngorongoro ili kuwakuza wanawake kiuchumi huku akitaja miradi
mingine iliyofadhiliwa na Oxfam kuwa ni pamoja na ujenzi wa maghala ya
kuhifadhia chakula, ujenzi wa majosho, pamoja na ujenzi wa vyanzo vya maji.
uliowashirikisha wanawake wa vijiji hivi vinne walituambia kwamba wanahitaji
vituo vya kusindika na kuhifadhia maziwa. Tumewajengea vituo hivi mvitumie kwa
maendeleo yenu.” Stellah pia aliipongeza serikali na wadau mbalimbali kwa kutoa
ushirikano mkubwa uliopelekea kufanikisha ujenzi wa vituo hivyo ikiwemo kutoa maeneo
ya ardhi ya vijiji hivyo vinne.
kibiashara na kuepuka kutegemea mashirika na taasisi ambazo zipo kwa muda tu.
uwezo wana vikundi hao kwa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na mbinu mbalimbali
za kibiashara pamoja na kuwafundisha namna za kutunza maziwa kwa usafi.
na waweze kunufaika kwa namna mbalimbali ikiwemo kupatiwa mikopo na kufungua
akaunti ya benki
kuuza maziwa na siagi.
mwanamke ambaye nina watoto watano na sina mume natarajia kutumia kipato
kutokana na biashara hii kusomesha watoto.
120 na kila kimoja kina jokofu linalotumia umeme wa jua, mashine za
kusindika maziwa, madumu ya kuhifadhia maziwa, vipima joto, vipimo vya kupimia ubora wa maziwa, tenki la maji pamoja na mashimo mawili ya vyoo na bafu.
Shirika la Oxfam labidhi vituo vya kusindika na kuhifadhi maziwa ngorongoro
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 21, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment