Mchezaji wa timu ya wanawake ya Nigeria Ugo Njoku amepigwa marufuku ya mechi tatu.
Kamati
ya nidhamu ya FIFA ilifanya kikao chake nchini Canada na kufikia uamuzi
huo baada ya kutizama video inayomuonesha Njoku akimpiga kumbo mchezaji
wa Australia Sam Kerr katika mechi ya makundi ya kombe la dunia la
wanawake .Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa mchezaji wa akiba na aliingia uwanjani katika dakika ya 52 ya mechi hiyo ya kombe la dunia.
Japo tukio hilo halikuonekana na muamuzi wa mechi hiyo, kamati hiyo ya nidhamu ilikaa kandokando ya kombe la dunia na kufikia uamuzi huo.
Mchezaji huyo amepigwa faini ya dola elfu tatu na mia mbili $3,200.
The Super Falcons ya Nigeria iliambulia kichapo cha mabao 2-0 katika mechi hiyo.
Njoku sasa hataruhusiwa kushiriki mechi dhidi ya Marekani.
Haijulikani kwanini hatua sawa na hiyo haikuchukuliwa dhidi ya mshambulizi wa Ufaransa Camille Abily aliyempiga kumbo mlinzi wa England Laura Bassett.
FIFA yampiga marufuku Kiungo wa Nigeria
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 15, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment