Naibu waziri wa Fedha, Mwigulu Lameck Mchemba ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi ametangaza nia ya kuomba ridhaa ya wana Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumteua kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakao fanyika nchini kote baade mwaka huu.
Mwana siasa hiyo ambaye kwa siku za hivi karibuni amejizolea sifa kutokana na kauli zake amesema kipaumbele chake ni kujenga uchumi na kuwafanya watabnzania kumiliki uchumi wao.
Nchemba akitangaza nia hiyo leo katika Chuo cha Maendeleo ya Mipango mjini Dodoma akisindikizwa na familia yake ya mke na watoto watatu amesema pia kuwa lengo la kutangazia Dodoma ni mwanzo tu wa harakati za kuhamia Dodoma kwa serikali yake pindi akiingia madarakani.
Aidha Nchemba alisema mtu anayetaka kuongoza watanzania ni lazima atambue ajenda za Watanzania, ayatambue mazingira ya Watanzania na kama hajabeba ajenda ya Watanzania, basi uongozi wake hautakuwa wa wananchi.
MWIGULU MCHEMBA AUNGURUMA DODOMA AKITANGAZA NIA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 15, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment