Watu nane wafa kwa mvua Dar es Salaam



 Watu nane wamekufa na mamia kukosa makazi kutokana na mvua kubwa zinazonyesha katika jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau aliyepo jijini Dar es Salaam mvua hizo zimekuwa zikinyesha mfulullizo na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu pamoja baadhi ya watu kukosa makazi yao.

Kumekuwa na foleni kubwa ya magari na baadhi ya watu wamechelewa kwenda na kurudi kazini.
Mamlaka ya hali hewa nchini imetahadharisha kuwa mvua hizo zinaweza kuendelea japo zitapungua kidogo.
Watu nane wafa kwa mvua Dar es Salaam Watu nane wafa kwa mvua Dar es Salaam Reviewed by KUSAGANEWS on May 08, 2015 Rating: 5

No comments: