MWIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI ENG, CARLOS MKUNDI ATOA POLE KWA WAHANGA WA MAFURIKO


Mwimbaji wa nyimbo za injili Eng Carlos Mkundi ametoa pole kwa wahanga wa mafuriko nchini hususani kwa wakazi waishio Dar es salaam.

Mwimbaji  huyo anayetamba kwa kibao chake cha NIMETOKA MBALI  Ametoa wito huo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  kufuatia mafuriko yaliyoleta athari kubwa Mangwe jijini Dar es salaam na kuua watu kumi na moja na wengine kukosa makazi

Eng Carlos amewasihi watumishi wa Mungu kote nchini kuiombea Tanzania dhidi ya majanga mbalimbali yanayoendelea kama ajali na mafuriko na kuwatia moyo  walioathiriwa na mafuriko jijini Dar Es Salaam


Amesema watanzania wote kwa kushirikiana na watumishi wa Mungu pia  hawana budi kumwomba Mungu alete Mvua ya kiasi itakayowezesha kuotesha mimea kwa ajili ya mazao

Hata hivyo ameitaka serikali kutoa elimu ya kotosha kwa watu waishio mabondeni na kuwatafutia maeneo mazuri  ili kupunguza maafa ya mafuriko hapa nchini
Mafuriko yanazidi kuwa tishio kwa maisha ya watanzania walio wengi hasa kwa mikoa ya Dar Es Salaam, Morogoro na shinyanga.
MWIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI ENG, CARLOS MKUNDI ATOA POLE KWA WAHANGA WA MAFURIKO MWIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI ENG, CARLOS MKUNDI ATOA POLE KWA WAHANGA WA MAFURIKO Reviewed by KUSAGANEWS on May 12, 2015 Rating: 5

No comments: