Miongoni mwa matatizo hayo ni lile lililoelezwa kuwa katika kipindi cha mwaka 1966 na 1992 walitoweka mbwamwitu wengi katika hifadhi hiyo na wengine wakihamia Hifadhi ya Ngorongoro na Maasai Mara nchini Kenya
Mbwamwitu ni miongoni mwa wanyamapori waliopo kwenye mkakati wa kuokolewa kutokana na hatari ya kutoweka kwenye hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Kubainika kuteketea kwa wanyama hao kuliibua utata kuhusu kilichosababisha tatizo hilo.
Miongoni mwa matatizo hayo ni lile lililoelezwa
kuwa katika kipindi cha mwaka 1966 na 1992 walitoweka mbwamwitu wengi
katika hifadhi hiyo na wengine wakihamia Hifadhi ya Ngorongoro na
Maasai Mara nchini Kenya.
Hata hivyo, watafiti wa mambo ya wanyamapori
wakasema kuhama huko siyo sababu kuu inayoweza kutumika kama kigezo cha
kupungua kwa mbwamwitu katika Mbuga ya Serengeti.
Sababu nyingine zikaelezwa ni magonjwa kwa wanyama walao nyama kama vile simba, dumu na chui.
Sababu nyingine ikatajwa ni kuwapo kwa mabadiliko
ya tabianchi na uoto wa asili na misitu kwa ujumla inapotea na matokeo
yake wanyama wanashindwa kupata hifadhi pamoja na chakula.
Sababu nyingine zinazozungumziwa ni huenda
kumekuwapo kwa hujuma kutoka kwa watafiti wa nje wa wanyama hao. Hii ni
kutokana na maelezo kuwa ongezeko la watafiti linakwenda sanjari na
kupungua kwa wanyama hao.
Hata hivyo, ripoti za karibuni zinaonyesha chanzo
ni migogoro kati ya jamii ya wafugaji na wanyama hao katika maeneo ya
Loliondo.
Mbwamwitu walikuwa wanaelekea kuisha katika
hifadhi hii, waliokuwa eneo la Loliondo walianza kuuawa kwa sumu
kutokana na migogoro na wafugaji.
Sababu za kuwaua zinaelezwa kuwa ni kutokana na wanyama hao kushambulia na kuua mifugo kama vile mbuzi na kondoo.
Hakukuwapo na jumuisho la moja kwa moja la sababu lakini Taifa likaona kuna umuhimu wa kukoa kizazi cha wanyama hao.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Allan Kijazi anasema
kutokana na umuhimu wa wanyama hao shirika limekuwa likijitahidi
kuwakamata na kuwahifadhi eneo maalumu ili waendelea kuzaliana
RAIS Kikwete Nitajitosa kuhifadhi wanyamapori baada ya kustaafu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 07, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment