Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Christopher Kangoye na diwani wa Kata ya Terat jijini hapa, Julius Ole Sekeyan wamemfagilia mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Philleon Mollel kuwa ndiye kiongozi anayetakiwa katika Jiji la Arusha sasa.
Wakati Kangoye akisema kwamba Mollel maarufu kama
Monaban amekuja kubadilisha maisha ya vijana wa Arusha, Ole Sekeyan
amesema mgombea huyo ndiye chaguo la Mungu.
Viongozi hao walitoa kauli hizo mwishoni mwa wiki
katika hafla ya uzinduzi wa Shule ya Msingi ya Losio iliyopo Kata ya
Terat jijini Arusha ambako mtia nia huyo alichangia mabati 50 na
matofali 1,000. Kangoye ambaye alialikwa kama mgeni rasmi katika tukio
hilo alisema kwamba Mollel amekuja kubadilisha maisha ya vijana wa
Arusha na kuwataka vijana kuacha kulalamika ovyo.
“Siyo mnamuona Monaban pale mnadhani amekuja hivi
hivi? Umetumika ushawishi mkubwa sana huyu amekuja kubadilisha maisha ya
vijana na vijana acheni kulalamika.
“Kamanda wa UVCCM ni nafasi kubwa sasa wewe
kamanda ni lazima uonyeshe utawafanyia nini wananchi wa Arusha wewe na
makamanda wenzako wa wilaya,” alisema Kangoye.
Hata hivyo, Ole Sekeya aliwataka wakazi wa Arusha kumwomba Mungu ili awape kiongozi bora atakayeshughulikia matatizo yao.
huku akimtaja Mollel kwamba ni aina ya kiongozi bora kwa kuwa anajitoa kusaidia wanyonge.
“Muda umefika wa watu kuona matokeo ya kazi yenu
ya maombi,tumuombe Mungu safari atupe kiongozi bora huyu Phillemon
ameanza kazi miaka mingi kusaidia umma mimi nilimfuata mwaka 2000
atusaidie kupaua kanisa la Pentecoste hakika Mungu ametuonyesha kiongozi
mzuri naye ni Phillemon”alisema Ole Sekeyan.
Kwa upande wake Mollel alisema kuwa maendeleo
yoyote ndani ya jamii husika huletwa na watu na watu wenyewe ndio sisi
na kuwataka wakazi wa kata hiyo kuchangia shughuli za maendeleo.
Mollel,ambaye aliendesha zoezi la uchangiaji wa
ujenzi wa shule hiyo alitangaza matokeo yake na kusema jumla ya kiasi
cha sh,laki 5 na ahadi ya sh,7 milioni zilipatikana huku matofali
1000,bati 50,shamba nusu heka pamoja na mbuzi wawili na kondoo mmoja
walipatikana.
DC Arusha amfagilia aliyetangaza nia CCM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 07, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment