Wananchi wa familia saba za kijiji cha Sakila kilichopo kata ya kikatiti wilayani Arumeru mkoani Arusha wanalala nje na watoto wao huku wakikabiliwa na njaa kali baada ya watu wanaodai kutumwa na serikali ya kijiji kuvunja nyumba zao na kufyeka migomba yao.
Wakizungumza na wandishi wa habari wananchi hao wanaodai kuwa wameishi maeneo hayo
kwa zaidi ya miaka 30 wamesema wanashangazwa na viongozi wa kijiji
hicho kutoa baraka za kuvunja kwa nyumba zao kwa kisingizio kwamba wao
ni wavamizi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Richard Mbise amesema hatua hiyo
imekuja baada ya mahakama kuthibitisha kuwa wananchi hao walivamia eneo
hilo na walikiuka taratibu.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wastaafu wa vijiji vya kata hiyo
pamoja na kukiri kuwepo kwa mgogoro huo wamesema hatua ya
zinazochukuliwa kuutatua zikiwemo za kuvuja nyumba na kukata migomba
sio sahihi.
Tatizo la migogoro ya ardhi katika wilaya ya Arumeru ambalo kwa
sasa linaelekea kuwa sugu limeendelea kuwaathiri wananchi wa huku
baadhi ya viongozi wakiwemo wa kisiasa wakilitumia kama ajenda za
kutafuta maslahi yao jambo ambalo lisipodhibitiwa linaweza kuleta maafa
makubwa.
Wananchi walala nje na watoto baada ya nyumba na mashamba yao kufyekwa mkoani Arusha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 12, 2015
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 12, 2015
Rating:


No comments:
Post a Comment