Chama cha demokrasia na maendeleo -Chadema kimewataka watanzania kutambua, dawa ya migomo na migogoro kwenye sekta mbalimbali inayoendelea nchini ni kuiondoa CCM madarakani kupitia umoja wa katiba wa wananchi–UKAWA kwenye uchanguzi mkuu ujao, kwa kuwa imeshindwa kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya wananchi.
Hayo yamesemwa na naibu katibu mkuu wa chama hicho John Mnyika
kwenye mkutano wa uchanguzi wa viongozi wa kanda ya kusini wa chama
hicho uliofanyika mkoani Mtwara, na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi
mbalimbali wa Chadema toka mikoa ya Mtwara na Lindi, katika kutekeleza
sera ya majimbo kwa mujibu wa katiba mpya ya chama hicho ambapo
ulichagua mwenyekiti wa kanda, makamu mwenyekiti, mratibu wa kanda,
afisa wa kanda na kamati 6 za utendaji za kanda hiyo ya kusini katika
kuimarisha chama na kujiandaa na uchaguzi mkuu ujao.
Naibu katibu mkuu huyo wa Chadema John Mnyika amesema, taifa
linapita kwenye migogoro na migomo inayoathiri uchumi na ustawi wa
wananchi, na hivyo dawa ya kumaliza migomo na migogoro hiyo ni kuiondoa
CCM madarakani kwenye uchaguzi mkuu ujao huko akidai umoja wa katiba ya
wananchi - UKAWA ipo imara kutekeleza matarajia ya wananchi katika
kushinda uchaguzi mkuu ujao.
Aidha baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa uchaguzi wamewataka
wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye
daftari la kudumu la kupigia kura wakati utakapowadia, ili kufanikisha
malengo ya chadema na umoja wa katiba ya wananchi ukawa wa kushinda
kwenye uchaguzi mkuu ujao yaweze kufanikiwa.
Chadema kimewataka watanzania kutambua dawa ya migomo na migogoro inayoendelea nchini.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 12, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment