Waandishi wa habari walifika katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam
majira ya asubuhi na kushuhudia mabasi ya abiria yakiwa yameegeshwa
ambapo baadhi ya abiria waliotegemea kusafiri wameeleza adha
walizokutana nazo.
Baada ya madereva kuendelea kushikilia msimamo wao wa kugoma,
baadhi ya madereva wa bodaboda waliokuwa wakipita na abiria katika
barabara ya Morogoro walianza kufukuzwa na kundi la vijana ili kuwapiga
huku matairi ya magari yakichomwa moto ili kuzuia magari kutumia
barabara ya Morogoro.
Kurushiwa mawe kwa askari wa jeshi la polisi ilisababisha mabomu ya
machozi kuanza kupigwa hewani hali iliyosababisha watu kukimbia
ovyoovyo huku baadhi ya walemavu wakiishiwa nguvu.
Umati wa watu walikuwa katika eneo hilo waliendelea kuzuia magari
ambapo jeshi la polisi ikamua kuongeza nguvu kwa kuleta magari ya maji
ya washa washa, gari la jeshi la wananchi Tanzania lakini jitihada hizo
zilipoonekana kushindwa kuondoa makundi ya watu ndipo mabomu yakaanza
tena kupigwa.
Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam alilazimika kufika
katika kituo cha Ubungo akiongozana na viongozi wa mkoa wa Dar es
Salaam ambapo baada ya madereva hao kulazimisha kuzungumza na mawaziri
husika, kamishna Kova alifanikiwa kumpata waziri wa kazi na ajira Mh
Gaudencia Kabaka ambapo kabla ya waziri kuzungumza viongozi wa madereva
hao wakaeleza madai yao sita.
Katika kumaliza mgomo huo kutoendelea, kamishna Kova akakiri
kuthibiti askari wake kutoendelea kusumbua madereva huku waziri wa kazi
na ajira Mh Kabaka akikiri kuingilia kati ili kumaliza madai ya madereva
hao.
Baada ya waziri kuwaridhisha madereva hao, madereva walianza
kuruhusu abiria kuingia ndani ya mabasi kwa ajili ya safari kuanza ikiwa
ni majira ya saa7 na nusu mchana.
Serikali yakubali kutatua madai ya madereva kumaliza mgomo nchini.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 12, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment