City wanasema hawatishwi na maneno ya Yanga na wamejipanga kuhakikisha wanapunguza kasi ya vinara hao Jumapili kwa kuwafunga na kurudi na pointi tatu Jijini Mbeya
TIMU ya Mbeya City, imesema haitishwi na Yanga licha ya kutoa kipigo cha mabao 8-0 kwa Coastal Union Jumatano iliyopita uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Msemaji wa Yanga Jerry Muro ameimbia Goal kuwa Mbeya City wajiandae na kipigo kikubwa zaidi ya walichoipa Coastal Union Jumatano iliyopita kutokana na kasi waliyokuwa nayo hivi sasa kuelekea ubingwa wa Tanzania bara msimu huu.
Msemaji wa Mbeya City Dismas Tem, amesema hawatishwi na maneno ya Yanga na wamejipanga kuhakikisha wanapunguza kasi ya vinara hao Jumapili kwa kuwafunga na kurudi na pointi tatu Jijini Mbeya.
“Sisi hatuna maneno mengi tusubiri baada ya dakika 90 ndiyo tutaona nani mkweli najua Yanga ni timu nzuri na kubwa na wapo kwenye ubora wa juu kwa sasa lakini mpira unachezwa uwanjani siyo mdomoni,”amesema Dismas.
Mbeya City wajiandae na kipigo kikubwa kuliko cha Coastal’ Jerry Muro
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 18, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment