waziri wa Mapatano ya Kitaifa wa Mali amesema kuwa serikali ya nchi hiyo haitafanya mazungumzo na makundi yanayobeba silaha nje ya fremu ya makubaliano ya amani ya Algeria. Zahabi Ould Sidi Mohammed,
Waziri wa Mapatano ya Kitaifa wa Mali amesema katika makubaliano yaliyosainiwa kati ya serikali na wapinzani huko Algeria, serikali ya Mali imewapatia wakazi wa maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo haki kamili na haki ya kujiendeshea masuala yao kieneo kupitia chaguzi za mabaraza ya miji na chini ya usimamizi wa Bamako. Sidi Mohammed amesisitiza kwamba:
Serikali ya Mali itafanya mazungumzo na wapinzani katika fremu ya makubaliano yaliyosainiwa na pande mbili hizo mwezi Machi uliopita huko Algeria na kwamba kwa mujibu wa makubaliano hayo, matatizo na migogoro mingi itapatiwa ufumbuzi. Waziri wa Mapatano ya Kitaifa wa Mali ameongeza kuwa hakuna eneo linalojulikana kama eneo lililojitenga la Azawad na wakazi wa kaskazini mwa nchi hiyo pia wanapinga Azawad kujulikana kwa jina hilo.
Amesema kwa msingi huo maoni ya wananchi pia yanapaswa kuzingatiwa katika suala la kuipa majina mikoa ya kaskazini mwa Mali.
Mali yataka mazungumzo katika fremu ya makubaliano
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 06, 2015
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 06, 2015
Rating:


No comments:
Post a Comment