Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametaka zichukuliwe sera za pamoja za nchi za eneo la Afrika Mashariki kwa shabaha ya kukabiliana na vitisho vya ugaidi vinavyoendelea kutikisa nchi mbalimbali za Kiafrika.
Kwenye hotuba aliyoitoa jana usiku, Rais Museveni amesisitiza kwamba vita dhidi ya ugaidi vinapaswa kutekelezwa kwa ushirikiano wa nchi zote za eneo hilo. Rais wa Uganda amesisitiza kwamba wakati umefika kwa viongozi wa nchi za eneo la ukanda wa Afrika Mashariki kuchukua mkakati mmoja wenye lengo la kutokomeza mashambulio ya kigaidi na makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka.
Rais Museveni ameongeza kuwa, juhudi kubwa zinapaswa kuchukuliwa kwa lengo la kukabiliana na makundi hayo hadi pale yatakapotokomezwa kikamilifu. Nchi za Somalia, Nigeria, Niger, Cameroon, Kenya na Chad zinakabiliwa na mashambulio ya mara kwa mara ya makundi ya kigaidi.
Hivi karibuni magaidi wa kundi al al Shabab la nchini Somalia walitekeleza shambulio la kigaidi dhidi ya wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya, na kusababisha watu wasiopungua 150 kuuawa, na mamia ya wengine kujeruhiwa.
Rais Museveni EAC iweke mkakati dhidi ya magaidi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 06, 2015
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 06, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment