Jaji mmoja nchini Argentina ametoa
agizo la kukamatwa kwa mwanamuziki Justin Bieber siku ya ijumaa akisema
kuwa mwimbaji huyo alikataa kufika mbele yake kuhusiana na madai kwamba
aliwaagiza walinzi wake kumshambulia mpiga picha mmoja mwaka 2013.
Ujumbe uliotumwa kwa Bieber haukujibiwa mara moja.
Bieber anashtumiwa kwa kuwatuma walinzi hao kumshambulia mpiga picha Diego Pesoa nje ya kilabu moja ya Bueno Aires.
Msanii huyo hatahivyo hakurudi nchini Argentina ili kujibu maswali kuhusu kisa hicho.
Chini ya sheria za Argentina Bieber atakabiliwa na kifungo cha kuanzia mwezi mmoja hadi miaka sita jela iwapo atapatikana na hatia ya shtaka la kumjeruhi mpiga picha huyo.
Jaji ataka Justin Bieber akamatwe
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 11, 2015
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 11, 2015
Rating:


No comments:
Post a Comment