HAYA NDIO MAMBO YA UCHUMI BULUU!


 

Waziri Mkuuu , Kassim Majaliwa akifurahia na waoneshaji wa bidhaa zitokanazo na uwekezaji katika uchumi wa buluu leo Septemba 11 akimuwakilisha Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Umoja wa Nchi za Afrika ,karibian na Pasifiki (OACPS )Wanaohusika na masuala ya Uvuvi ,Bahari ,Maziwa na Mito ,kwenye Kituo  cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerer  jijini Dar es Salaam ..


Malengo ya mkutano huo ni kuimarisha utekelezaji wa Makubaliano yaliyofikiwa ;kuimarisha utekelezaji wa vipaumbele vya kimkakati vya umoja ;kubadilishana uzoefu ;kuweka mikakati ya pamoja ;na kuimarisha ushirikiano na washirika ili kuboresha usimamizi wa bahari ,uchumi wa buluu na maendeleo endelevu ya uvuvi .


Aidha Mkutano  huo unatarajiwa kutoa mwongozo wa kimkakati kwenye vikao vya juu vya maamuzi vya umoja wa Nchi za Afrika ,Karibian na Pasifiki kuboresha usimamizi wa bahari ,uvuvi na ufugaji wa samaki endelevu.

HAYA NDIO MAMBO YA UCHUMI BULUU! HAYA NDIO MAMBO YA UCHUMI BULUU! Reviewed by KUSAGANEWS on September 11, 2024 Rating: 5

No comments: