Katibu Mkuu wa CCM ,Dk Emmanuel Nchimbi amesema chama hicho kimeanza mazungumzo yasiyo rasmi na vyama vya Upinzani vikiwemo Chadema na ACT -Wazalendo .
Dk Nchimbi amesema hayo leo Ijumaa,Septemba 13,2024 ofisi ndogo za CCM ,Lumumba jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari .
Mtendaji mkuu huyo amesema hayo yote wakati akijibu swali aliloulizwa juu ya umuhimu wa mazungumzo baina ya CCM na vyama vingi ili kudumisha kuaminiana na amani ya nchi.
Amesema kuna mazungumzo yasiyo rasmi yanayoendelea na anafanya yeye mwenywe kwa lengo la kupata mwafaka wa Taifa .
Dk Nchimbi amesema hata washiriki wa mazungumzo hayo nupande wa CCM watachagua wale wenye nia na lengo zuri la mazungumzo kwani baadhi 'Ukiwaona tu anavyozungumza unaona huyu hafai ,tutachagua wenye engo la maridhiano'.
'Kwa upande wetu ,tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha mazungumzo yanakuwepo'amesema Dk Nchimbi.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 13, 2024
Rating:


No comments:
Post a Comment