Jumla ya sh1.29 billion zitatumika kuwalipa fidia wakazi 724 wakiwamo wa Muhambwe mkoani Kigoma wanaotakiwa kupisha ujenzi wa barabara kutoka kibondo hadi Mabamba .
Waziri wa Ujenzi , Innocent Bashungwa amesema hayo leo Septemba 3,2024 wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Muhambwe (CCM)Dk Florence Samizi.
Mbunge huyo amehoji ni lini Serikali itawalipa fidia wananchi wa Muhambwe waliopisha ujenzi wa Barabara ya Kibondo hadi Mabamba .
Akijibu swali hilo,Bashungwa amesema Serikali imekamilisha tathmini ya mali nza wananchi zitakazoathiriwa na mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kibando -Mabamba yenye urefu wa kilometa 47,925
Bashungwa amesema sasa Serikali inakamilisha taratibu za malipo ya fidia kwa wananchi hao,Amesema baada ya shughuri hiyo kukamilika wananchi hao watalipwa fidia .
BILIONI 1.29 KULIPWA FIDIA KWA WAKAZI 724 KIGOMA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 03, 2024
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 03, 2024
Rating:


No comments:
Post a Comment