WAZIRI MASAUNI AKUTANA NA WAKUU WA POLISI KUJADILI USALAMA NA AMANI.


 

Waziri wa mambo ya Ndani wa Tanzania ,Hamad Masauni  leo Jumanne ,Agosti 27,2024 amekutana na kufanya kikao na uongozi wa Jeshi la Polisi ukiongozwa na Inspekta  Jwenerali wa Poisi (IGP),Camillus Wambura jijini Dodoma.


Kikao hicho kimehusu masuala ya usalama na amani ya nchi ikiwemo kujadili matukio ya kiuhalifu yanayotokea sehemu mbalimbai nchini na hatua zinazochukuliwa kuendeea kudhibiti matukio hayo.


Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Daniel Sillo ,Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dk Maduhu Kazi ambapo kwa upande wa Jeshi la Polisi kimehudhuriwa na viongozi  mbalimbai akiwemo kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimaliwatu,Suzan Kaganda .


Kamishna wa Fedha na ojistiki,Liberatus Sabas,Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ,Awadh Juma ,Kamishna wa Sayansi ya Uchunguzi wa Jinai , Shabani Hiki ,Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhani Kingai.


Pia ,msemaji wa Jeshi la Polisi , David Misime, Naibu Kamishna kutoka Kamisheni ya Inteijensia na Jinai , Kheriyangu Khamis Mgeni ,Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Jumanne Muliro.

WAZIRI MASAUNI AKUTANA NA WAKUU WA POLISI KUJADILI USALAMA NA AMANI. WAZIRI  MASAUNI AKUTANA NA WAKUU WA POLISI  KUJADILI USALAMA NA AMANI. Reviewed by KUSAGANEWS on August 27, 2024 Rating: 5

No comments: