ALIYEDAI KUPIGWA HADI KUVUNJWA MGUU NA KIGOGO WA POLISI ARUSHA, AMEDAI KUPOKEA VITISHO VYA UHAI WAKE
Mkazi wa kata ya Daraja Mbili jijini Arusha aliyedai kupigwa hadi kuvunjwa mguu na askari wa jeshi la Polisi ,amedai kupokea vitisho vya kukatishiwa uhai wake.
Peter alidai amevunjwa mguu ndani ya chumba cha mahojiano kilichopo ndani nya kituo cha polisi jijini Arusha Juni 6,2024 akilazimishwa kukubali kosa la kucheza kamari baada ya kukamatwa na askari watatu akiwa nyumbani kwao usiku .
Hata hivyo ,Jeshi la Polisi Mkoani huko limemtaka kutoa taarifa kuhusu vitisho hivyo ili zifanyiwe kazi.Akizungumza leo Agosti 21,2024 ,Peter amesema baada ya kutoa taarifa kwa mwandishi wa habari ,amekuwa akipokea vitisho vingi kutoka kwa watu asiowafahamu.
Peter amesema baada ya vitisho hivyo amekuwa na hofu kubwa ya maisha yake na kuliomba Jeshi la Polisi kuharakisha upelelezi wa kesi yake ili watuhumiwa waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwa hatma ya watu wengine.
akizunguzma suala hili,Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ,SACP Justine Masejo amesema kuwa upelelezi wa suala hilo unaendelea ukikamilika utafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili lichukuliwe hatua zaidi .

No comments:
Post a Comment