Mwalimu wa shule ya msingi mbaroni kwa kuchoma tumbo la mpenzi wake shinyanga


Mwanamke aitwae Neema Kabulu (19) amenusurika kufa baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za usoni, tumboni,mkononi na Mwalimu Joseph Msafiri wa Shule ya Msingi Namagubu iliyoko Ukerewe Mkoani Mwanza ambaye ni mpenzi wake. 

Kwa Mujibu wa taarifa ya Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao kwa vyombo vya habari,tukio hilo limetokea Septemba 6,2019 majira ya saa nne kamili usiku katika maeneo ya Old Shinyanga, Kata ya Old Shinyanga, Tarafa ya Shinyanga Mjini, Manispaa ya Shinyanga.

"Neema Kabulu mkazi wa Ukerewe mkoani Mwanza alijeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za usoni, tumboni na mkono wa kulia na Joseph Msafiri ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Namagubu iliyoko ukerewe Mkoani Mwanza, ambaye ni mpenzi wake",ameeleza Kamanda Abwao.

"Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi. Majeruhi anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga na hali yake ni mbaya. Mtuhumiwa amekamatwa",ameongeza.
Mwalimu wa shule ya msingi mbaroni kwa kuchoma tumbo la mpenzi wake shinyanga Mwalimu wa shule ya msingi mbaroni kwa kuchoma tumbo la mpenzi wake shinyanga Reviewed by KUSAGANEWS on September 08, 2019 Rating: 5

No comments: