Na Ahmed Mahmoud Arusha
Serikali imelitaka shirika la
kimataifa ,Elimu ,Sayansi na Uchumi (UNESCO)kutoa takwimu sahihi juu ya matukio
ya waandishi wa habari kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji na mauaji kwa kila
nchi tofauti na kutoa takwimu za jumla ili kuangalia ukubwa wa jambo hilo kwa
kila taifa.
Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na
Michezo,Dkt ,Harrison Mwakyembe ameyasema hayo katika mkutano wa kimataifa
unaowashirikia waandishi wa habari kutoka nchi za ukanda wa kusini mwa jangwa
la sahara (SADC)katika siku ya kutathmini vitendo vya unyanyasaji na mauaji
dhidi ya waandishi wa habari dunia uliondaliwa na Unesco jijini hapa.
Amesema takwimu zilizotolewa na
UNESCO zinazoonyesha kuwa waandishi wa habari wapatao 1010 waliuawa katika
kipindi cha miaka 10 iliyopita,jambo ambalo halifafanui kiwango cha ukubwa kwa
Kila nchi zilizokumbwa na Kadhia hiyo .
Aidha amesema kuwa Umoja wa mataifa
umetenga siku ya Tarehe 2 kila mwaka kuadhimisha siku ya kupinga vitendo vya
unyanyasaji,uzalilishaji na mauaji kwa wanahabari kote ulimwenguni lakini
matatizo hayo yamekuwa yakijirudia bila kuyapatia ufumbuzi jambo ambalo ametaka
takwimu za kila nchi zikabainishwa ikujua uwiano ili kupima ukubwa wa tatizo.
Awali akiongea kwenye mkutano huo
Mkurugenzi wa Unesco Kanda ya Afrika mashariki Johnbosco Mayiga amesema kuwa
katika kipindi cha miaka kumi jumla ya wanahabari wapatao 1010 waliuawa katika
nchi mbali mbali duniani na hivyo kuongeza ukubwa wa vitendo vya ukatili kwa
wanahabari kukosa uhuru na usalama wawapo katika utekelezaji majukumu yao.
Katika Mkutano wa Unesco uliofanyika
mwaka jana jijini Nairobi uliazimia kila nchi kuangalia utaratibu gani wa
kufanya ili kuwajengea mazingira mazuri ya utendaji kazi kwa waandishi wa
habari ikiwemo kuwa na chombo cha kuwalinda.
Pamoja na Mambo mengine mkutano huu
utalenga kuangalia utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa Nairobi ikiwemo ni
hatua zipi ziweze kuchukuliwa katika kuhakikisha muandishi wa habari
anatekeleza majukumu yake katika mazingira salama.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa chama
cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (Tamwa) Bi Edda Sanga amesema kuwa
kitu alichokipenda katika mkutano huo ni mgawanyo wa wa wajumbe na kuwa
mwandishi si elimu pekee na ujuzi wa kazi utakaosaidia utendaji kazi wake
Amesema kuwa vyombo vya habari vina
nguvu kubwa ya kutupeleka katika hatua kubwa ya maendeleo iwapo kutakuwa na
mazingira mazuri kwa wanahabari na kutekeleza majukumu yao kwa weledi .
Serikali Yataka UNESCO Kutoa Takwimu Za Mauaji Kwa Nchi Badala Ya Jumla
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment