Shirika la Reli Tanzania (TRC),
limeeleza kushtushwa na maiti ambazo zimekuwa zikiziokota mara kwa mara kwenye
njia ya reli.
Limesema kwa wiki iliyopita pekee
zimeokotwa maiti mbili kwenye njia hiyo ya reli maeneo ya Gongo la Mboto, Dar
es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa
Shirika hilo, Focus Sahani, alisema jana kuwa wahusika walizitupa maiti hizo
kwenye reli kama ujanja kuonyesha kwamba watu hao waligongwa na treni.
Alisema shirika hilo limekuwa
likiokota maiti kwenye reli hiyo kila mara vitendo ambavyo vinawashtua kwa kuwa
hawajui wahusika wanafanya hivyo kwa lengo gani.
"Sasa hivi kumejitokeza matukio
mengi tu unakuta wengine wamewekwa relini, watu wanamfanyia mtu kitu kibaya
huko wanamtupa kwenye reli ionekane kama amegongwa na treni," alisema.
Alisema maiti hizo hadi sasa
hazijafahamika zinatupwa na watu gani kwenye reli.
"Wanaua mtu huko wanamleta
kwenye reli wanamuacha hapo ili kuonyesha kuwa amegongwa. Wanafanya hivi ili
kuondoa ushahidi wiki iliyopita peke yake tumeokota maiti mbili na matukio ya
aina hii yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara," alisema
Maiti Zaendelea Kuokotwa Kando ya Reli Dar
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment