Video vixen, Amber Rutty
amesomewa makosa mawili ikiwemo kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
Mbali na Amber Ruty washtakiwa
wengine ni Said Bakary Mtopali na James Charles maarufu kama ‘James Delicious’.
Kwa pamoja washtakiwa wamesomewa
mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustino Rwezire na wakili wa
serikali Nassoro Katuga.
Wakili Katuga amedai kuwa kosa la
kwanza ni kufanya mapenzi kinyume na maumbile ambalo linamkabili Amber Ruty.
Inadaiwa ametenda kosa hilo kati ama
baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary Mtopali kumuingilia
kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.
Pia kosa jingine la kufanya mapenzi
kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary Mtopali ambapo
anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya
mapenzi na Amber Ruty kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.
Kosa la tatu la kuchapisha video ama
picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa
kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.
Kosa jingine la nne ni kusababisha
kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruty na Said Abubakary Mtopali ambapo
wanadaiwa kati October 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia
makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kweli.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo,
Wakili Katuga amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika wanasubiri
taarifa za Kitaalamu kuhusu picha hizo za ngono za minato.
Washtakiwa wamepatiwa masharti ya
dhamana ya kuwa na wadhamini 2 kila mtu na kusaini bondi ya Shilingi Milioni
15.
Pia wadhamini wawe na vitambulisho
vya taifa pamoja na kuwasilisha hati zenu za kusafiria na msitoke nje ya Dar es
Salaam bila ruksa.
Hata hivyo mshtakiwa James Delicious
aliyefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana, huku Amber Ruty na Said Bakary
Mtopali wameshindwa kutimiza masharti na kupelekwa gerezani.Kesi imeahirishwa
hadi November 12,2018.
James Delicious Kadhaminiwa....Amber Rutty Na Bwana Yake Wamekosa Dhamana na Kupelekwa Gerezani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment