Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi
wa Chama Cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe amedai makosa anayoshtakiwa
yanafanana na makosa ambayo walishawahi kushtakiwa baadhi ya waasisi wa bara la
Afrika.
Kwa mujibu wa Zitto Kabwe, amedai
kuwa kesi za namna hiyo ndizo zilizowahi kuwakumba baadhi ya waasisi, akiwemo
muasisi wa Taifa la afrika kusini, Nelson Mandela pamoja na muasisi wa
Tanzania Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza mara baada ya kupatiwa
dhamana, Zitto Kabwe amesema ; “kesi za namna hii wamefungwa wakina mandela,
na mwalimu kwa hiyo sio jambo linalopaswa kuwatisha watu. Ila nasikitika sana
jana sikushiriki kongamano la chuo kikuu cha Dar es salaam.
“Naamini lazima tuweze kutoa tafsiri
mbadala juu ya kile kilichotokea jana, pia niwatake watanzania tuwe na
mshikamano ili kuhakikisha nchi yetu inakuwa imara.”
Mbunge huyo wa Kigoma mjini
anashtakiwa kwa makosa matatu ya uchochezi, ambapo katika kesi yake upande wa
Jamhuri unawakilishwa na Wakili, Tumaini Kweka na upande mshtakiwa unawakilishwa
na wakili Peter Kibatala.
Zitto alikamatwa na Jeshi la Polisi
jijini Dar es salaam oktoba 31 mwaka huu kufuatia mkutano wake na waandishi wa
habari ambapo alitoa madai ya kuawawa kwa zaidi ya raia 100 katika Wilaya ya
Uvinza Mkoani Kigoma.
Kesi ya Mbunge huyo inatarajiwa
kuendelea tena Novemba 12 mwaka huu.
Alichokisema Zitto Kabwe Baada Ya Kuachiwa Kwa Dhamana Mahakamani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment