Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako amemuagiza katibu mkuu wizara hiyo kuwasimamisha kazi wakuu wa idara
ya fizikia na kemia wa Chuo cha Ualimu Morogoro
Ametoa uamuzi huo leo Agosti 8 wakati akizungumza na
wakufunzi wa chuo hicho kilichopo Morogoro ambapo wakuu hao wanadaiwa
kudanganya kuhusu matumizi ya vifaa vya maabara
Ndalichako amesema vifaa hivyo vilipelekwa katika chuo hicho
kutoka wizarani
Waliohusishwa na agizo hilo la waziri ni mkuu wa idara ya
fizikia, Noel Mgana na mkuu wa idara ya kemia, Josephat Temba ambao walishindwa
kumuelezea ukweli kuhusu kutotumika kwa vifaa vingi vya maabara ambavyo vingine
vinaelekea kuisha muda wake wa matumizi
Katika hatua nyingine ameagiza ofisa manunuzi wa wizara ya
elimu, Audifasy Myonga kusimamishwa kazi kwa kununua vifaa hivyo bila kuuliza
mahitaji halisi ya chuo na vifaa vingine kununuliwa kwa gharama kubwa zaidi
Waziri Ndalichako aagiza kusimamishwa kazi vigogo Chuo cha Ualimu Morogor
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 08, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment