Rais John Magufuli amefanya mabadiliko na uteuzi wa mkuu wa
wilaya mmoja na wakurugenzi 41 wa halmashauri za wilaya, miji na majiji
Katika mabadiliko yaliyotangazwa jana na Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi John Kijazi, Mkoa wa Dar es Salaam umebadilishiwa wakurugenzi
wa halmashauri za manispaa nne za Temeke, Ilala, Kigamboni na Ubungo
Halmashauri ambazo hazijaguswa katika mabadiliko hayo ni
Manispaa ya Kinondoni na Jiji la Dar es Salaam
Katika mabadiliko hayo, aliyewahi kuwa mkurugenzi mtendaji
wa Halmashauri ya Kinondoni, Mussa Natty ameteuliwa tena katika nafasi hiyo
kituo chake cha kazi kikiwa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduma
Wateule wapya mkoani Dar es Salaam ni Lusubilo Mwakabibi
(Temeke), Beatrice Kwai (Ubungo), Jumanne Shauri (Ilala) na Ng’wilabuzu
Ludigija (Kigamboni).
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aaron Kagurumjuli na
Mkurugenzi wa Jiji, Siporah Liana wanaendelea na majukumu katika nafasi zao
Aidha, mabadiliko hayo mkoani Dar es Salaam yamekuja wiki
moja baada Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, George Mkuchika kufanya uteuzi wa makatibu tawala wa wilaya 18
kujaza nafasi zilizokuwa wazi na kuwahamisha wawili
Katika mabadiliko hayo, ya makatibu tawala wa wilaya ya
yaliyofanywa Agosti 5, Hashim Komba aliyekuwa Temeke alihamishiwa Wilaya ya
Iringa na Edward Mpogolo wa Ilala alipelekwa Wilaya ya Dodoma. Nafasi ya DAS wa
Kinondoni iliyokuwa wazi ilijazwa na Stella Msoffe
Mabadiliko yaliyotangazwa jana ni ya tatu kwa wakurugenzi wa
halmashauri
Julai 7, 2016, Rais Magufuli alifanya mabadiliko ya kwanza
ya wakurugenzi kwa kuteua wa majiji matano, manispaa 21, miji 22 na wilaya 137
za Tanzania Bara. Kati ya wakurugenzi 185 walioteuliwa, 120 walikuwa ni wapya
na wengine 65 walikuwa wa zamani
Mabadiliko ya pili ya wakurugenzi yalifanyika Septemba 10,
2016 na Rais Magufuli alifanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya
11, mkurugenzi mmoja wa halmashauri ya mji na mkurugenzi mmoja pia wa
halmashauri ya manispaa
Aidha jana, Dk Kijazi pia alitangaza uteuzi wa Mkuu wa
Wilaya ya Kwimba, Senyi Ngaga ambaye amechukua nafasi ya Simeon Msafiri
aliyehamishiwa wilaya ya Chato
Alisema wakurugenzi ambao katika mabadiliko hayo
wamebadilishiwa vituo vya kazi wanapaswa kwenda kuripoti katika vituo vyao
vipya mara moja na ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza, watatakiwa kuripoti
kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)
jijini Dodoma kesho kwa ajili ya kupata maelekezo kuhusu majukumu yao na kula
kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma
Pia, Balozi Kijazi alisema wakurugenzi wateule wanaokwenda
Tamisemi wanapaswa kuwa na vyeti vyao halisi na nakala za vyeti hivyo
zilizothibitishwa kisheria vinavyoonyesha matokeo ya kumaliza elimu ya kidato
cha nne, kidato cha sita na taaluma zao
Wakati huohuo, Waziri
Mkuchika amemteua Mnkondo Bendera kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe kujaza
nafasi iliyoachwa wazi na Moses Mashaka ambaye amepangiwa kazi nyingine
Bendera anatakiwa kuripoti kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora jijini Dodoma kesho akiwa na
vyeti vyake halisi vya elimu ya sekondari na taaluma
Wakurugenzi wa halmashauri Dar wapanguliwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment