Wafanyakazi Mochwari wa Bugando wapewa ujuzi


Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza, imeanzisha mafunzo maalumu kwa wafanyakazi wa chumba cha kuhifadhia maiti

Mkuu wa Idara ya Maabara katika hospitali hiyo na Mkufunzi wa mafunzo hayo, Dk. Kahima Jackson,  amesema lengo la kuanzishwa kwa mafunzo hayo ni kutokana na watumishi wengi waliokuwepo kutokuwa na taaluma hiyo

'Tuliamua kuanzisha mafunzo haya baada ya kubaini kwamba watumishi wengi wa chumba cha maiti walikuwa wakitokea mitaani na kwamba hawana elimu inayohusiana na utunzaji wa maiti.' Amesema Dkt. Kahima Jackson

'' Nilichojifunza ni ule uchanganyaji wa dawa inayotumiwa kuhifadhi mwili, kule nilikokuwa nilikuwa nikiitumia bila ya kuchanganya, ni kali sana ilikuwa ikinichoma kwenye macho, inaniingia puani....'' Amesema Mhoja mmoja wa wahifadhi maiti katika mochwari ya hospitali ya Bugando

Licha ya kuhusika na utunzaji wa maiti, moja ya kazi yao pia ni kushirikiana na Daktari, pale uchunguzi unapohitajika kujua kiini ama sababu za kifo

Theophilda Ngojani mojawapo ya wanafunzi wakifuatilia kwa makini mafunzo

Kwa upande wake mwanamke pekee katika mafunzo hayo Theophilda Ngojani anasema watu walikuwa wakimchukulia kama mtu aliyechanganyikiwa kutokana na kufanya kazi hiyo

'Hii kazi ndio iliyotuweka mjini utakuta wote tunapanga foleni kutafuta mkate'. Amesema Theophilda.

Chanzo: BBC 

Wafanyakazi Mochwari wa Bugando wapewa ujuzi Wafanyakazi Mochwari wa Bugando wapewa ujuzi Reviewed by KUSAGANEWS on August 21, 2018 Rating: 5

No comments: